Jumatatu, 30 Oktoba 2017

NDANI YA DINI YANGU---3

AMEMKIRI KRISTO NA KUBATIZWA KWA MAJI MENGI {bofya kwa utangulizi}
Soma marko 16:15-17 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na pia warumi 10:9-10 {Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.}. kukiri kwa kinywa chako mwenyewe hii ndio hatua ya kwanza kabisa ya kuingia kwenye dini ya UKRISTO na siyo kwa kujikuta tu ndani ya ukristo. Kuna watu wamezaliwa babazao ni wachungaji au baba zao ni wazee wa kanisa Fulani wakaona kuwa kwasababu wamekulia kwenye mafundisho basi wao niwa KRISTO. Hapana mwajidanganya tu bure nafsi zenu inatakiwa umkiri KRISTO kwa kinywa chako mwenyewe tena mbele ya watu wengine kwamba mimi nitatembea na huyu KRISTO. Ukishamkiri unamkaribisha kuwa kiongozi wa Maisha yako kwa mda wote wa kuishi kwako. Kukiri kwa kinywa kwa maana ndogo ni kwamba unakubali kuwa kuanzia sasa mimi ni mtumwa wa YESU KRISTO katika mambo yote nakubali kuwa chini yake na nitajifunza magotini pake. Mungu wake ndio Mungu wangu Roho wake ndio Roho wangu na Maisha yake ndio Maisha yangu. Hapo ndipo unasema mimi ni mkristo. Baada ya hicho kitendo kinachofuata ni kubatizwa kwa maji mengi subiri niseme kidogo hapa kwamba kubatzwa siyo ishara bali ni ukamilisho kwa mtu yeyote aliyekubali kumfuata Yesu. Mathayo  3:13-15 soma vizuri hiyo mistari utaona kuwa kwenye msitari wa 15 Yesu mwenyewe anakiri kuwa ni haki na imetupasa wote kuitimiza. Nakuonya ndungu yangu sina ugomvi na mafundisho yenu wala dhehebu lako bali kama unataka kuwa MKRISTO hakika anza kutafuta kubatizwa kwa maji mengi na usikae tu kanisani bila kubatizwa omba kwa viongozi wako ubatizwe kwa maji mengi. Hakika usipobatizwa haki ya mbingu usipoitimiliza hauwezi kuiona mbingu hata kidogo kwa maana Yesu kaagiza kwenye mathayo 6:33{Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.}. kumbuka ubatizo ni haki ya ufalme wa mbinguni na siyo kwa mujibu wa kanisa Fulani. Kwasbabu ni haki ya mbingu yule mwenye kazi ndio anatakiwa kuonesha mfano na siyo kwa mjibu wa dhehebu Fulani tu. Yohana 3:22-23{Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.}. Tazama yohana aliyembatiza yesu alikuwa anabatiza kwenye maji tele. Sikia nikuambie kitu kimoja ndugu yangu katika KRISTO YESU ubatizo ulikuja kwa mkono wa Yohana ndio ambao biblia imeuagiza na sehem zote walipoagiza kubatiza au unapoona kubatizwa kwa maji ile siyo ishara tena bali ni agizo la ufalme wa mbingu. Ukitaka kujua kuwa ubatizo ulikuwa niwa aina moja muone towashi kwenye matendo 8:36-38. Hata pia wakati yesu anakuja kubatizwa yohana alikuwa anabatiza kwenye mto yordani. Basi kumbuka yesu anasisitiza kujifunza kutoka kwake kwenye mathayo 11:29-30 basi katika kujifunza kutoka kwa yesu  hakuna cha dhehebu langu limeagiza nini wala cha mchungaji wangu wala kiongozi wa dhehebu letu alikuwa na upako sana wala sijui alikuwa ni mmoja wa mitume au kaandika nyaraka zote maana hata yeye mwenyewe alifanya kubatiza kwa maji mengi pitia hata kwenye matendo ya mitume yote utaona watu wanabatizwa kwa maji tele kila sehem na hakuna sehem biblia imesema ni ishara tu. Basi ndugu achana na roho ya udini kabisaa jifunze kutoka kwa mwanzilishi wa Imani mwenyewe ambaye ni yesu KRISTO.

Mwandishi MICHAEL BASA 0765279698/+255789799199 
kama unaswali au ushauri au ombi nipigie au nitumie ujumbe mfupi{sms} kwa namba hizo utampata BASA mwenyewe na utapata vingi zaidi. Kwamaana Bwana ameniita kuwa mtumishi wako.  

Alhamisi, 26 Oktoba 2017

NDANI YA DINI YANGU ---2

 
   INAENDELEA..... {bofya hapa kusoma sehem iliyopita}
Kuna siku moja mtu mmoja aliniuliza Je BASA wewe kweli umeokoka? Nikamjibu HAPANA  unajua kwanini nilimjibu hivyo kwasababu sijafikia kwenye viwango vya wokovu ninavyovitaka na ambavyo biblia imeagiza mtu angalau kuvifikia tu kwa mawazo ya fikra yake. Kuwa mfuasi wa dini Fulani haishii kwenye jina wala kushiriki ibaada zao tu au kuhudum kwenye baadhi ya mikusanyiko ya dini hiyo. Kama hushiki sheria za dini yako hakika wewe siyo mfuasi wa hiyo dini bali ni mtu kama wasio wafuasi {KAFIRI}.
    Elewa kitu kimoja kwamba kuishi Maisha halisi ya dini yako kwa kufuata sheria za dini yako na miiko yake yote huko ndiko kuwa mwana dini wa hiyo dini yako. Ukiwa ni mwisilam hakikisha masharti ya uisilam unayafuata kwa kila kitu na kuitwa HAMIS siyo sifa ya wewe kuwa mwisilam kabisaa. Kuitwa LUKA haikufanyi wewe kuwa mfuasi wa KRISTO katika Maisha yako bali kuishi kwa mjibu wa maandiko ya kitabu chako au miongozo ya viongozi wa dini yako. Kwa mkristo Kuna madhara ya kuwa Mkrisito halafu humfuati kristo. Swali lako linaweza kuwa nitajijuaje kuwa namfuata Kristo na bado nipo kwenye njia sahihi ya kumfuta Kristo?. Kwamaana kuna watu ni wa Kristo kwa majina na madhehebu yao tu lakini kwa matendo Yesu hawajui watu hao. Kuna sifa za mtu anayemfuata Kristo kweli na siyo kwa maigizo kama watu wengi wanayofanya sasa kwamaana wameacha kazi ya msalaba na kujivika udini ambao Yesu hajaagiza hata kidogo. Hakuna Roho mtakatifu ambaye atashudia ndani yako akasema wewe niwa PENTEKOSTE au wewe niwa KATOLIKI au KKKT kama umefikia hapo wewe unajidanganya nafsi yako tu bure hakika humfuati Kristo bali umevaa roho ya udini. 
    Kama ukiweza kusema mimi niwa Kristo na matendo yako yakakiri kuwa wewe ni waKristo huyo ndio mtu ambaye ndani yake anadini ya UKRISTO. Kuna watu unawambia wewe hivyo unavyotenda ni kinyume na maadili ya dini. Anakujibu mimi si dini yako au mimi siyo dhehebu lako je hujui kuwa wizi ni dhambi je huji kuwa uongo ni dhambi?. Je ni dini gani iliyoagiza watu wasipendane au wasichukuliane katika makosa yao. Kuna watu wengine vinywa vyao vimejaa matusi na chuki wanatukana dini za wengine mara hivi mara vile. Lakini je dini yako inasemaje kuhusu kumfanya mwingine aawe dini moja nawe au kanisa moja dhehebu moja nawe?. Pia siyo kazi nyepesi kumfanya mtu mmoja atoke dini yake ya mda mrefu aje kwenye dini yako. Kuna sifa za MKRISTO aliye mfuasi wa KRISTO kweli nazo ni:-
  1. AMEMKIRI KRISTO NA KUBATIZWA KWA MAJI MENGI {bofya hapa kuisoma}
  2. AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU{bofya hapa kuisoma}
  3. AMEJIKANA KATIKA KUMFUATA KRISTO
  4. ANASHIKA SHERIA ZOTE PAMOJA NA SABATO ZOTE ZA BWANA
  5. ANADUMU NA KWELI SIKU ZOTE
  6. MATENDO YAKE HUMTANGAZA KRISTO{bofya hapa kuisoma }
  7. ULIMI WAKE UMEJAA UZIMA
  8. ANAIJUA KWELI NA HIYO KWELI IMEMUWEKA HURU
  9. HUCHUKIA DHAMBI KWA MATENDO YAKE 
Tutaaanza kujadili sifa moja baada ya nyingine kadiri BWANA atakavyotupa uzima na mda pia.

MWANDISHI MICHAEL BASA 0765279698/+255789799199

Jumapili, 22 Oktoba 2017

NDANI YA DINI YANGU

Watu wengi tuna dini zetu au kwa maana nyingine tuna mfumo wetu wa Maisha wenye miiko na sheria pia. Dini yako inaweza kuwa tofauti na ya mwingine au zikawa sawa. Kumbuka miiko ndio inayoifanya dini yako iweke watu waufanano mmoja pamoja kwa lengo moja. Ndani ya miiko yako ndipo lengo kuu huandaliwa kwaajili ya watu wote walio kwenye dini yako kutoa mda wao kwa nguvu zote ili kulifikia. Sheria ndani ya dini yako zipo kukufanya ubaki kwenye njia sahihi wakati unaenda kutimiza lengo la ndani ya dini yako. Swali siyo usahihi wa dini swali ni je bado upo kwenye njia sahihi ya kulifikia lengo la dini yako??. 
            Nataka nielezee lakini nitatumia Zaidi maandiko ya kwenye biblia maana ndiko niliko na maarifa mengi na mifano mingi. Ukisoma yakobo 1:26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Hapa tatizo siyo mtu kuwa na dini tatizo je hiyo dini yake ndio misingi ya Maisha yake?. Je ulimi wake unaua au unaponya? Soma mithali 21:23 na mithali26:28. Utagundua kuwa kama mtu ana dini yake anatakiwa ajifunze kuwa wa haki kwenye hiyo misingi na sheria za dini yake. Kuna watu wamekuwa wakijidanganya kuwa mimi ni dini Fulani wala siyo dini ile lakini matendo yake hayatupi picha ya ile dini anayoisema. Mtu anaweza kusema mimi ni mwisilam wakati hata sura moja hajui kusoma kwa picha sasa unajiuliza huyu dini yake kwa mawazo yake ni uislam lakini kwa matendo anakataa. Mwingine anaenda mbali Zaidi kwa kusema sisi tumezaliwa kwenye uislam lakini kuswali ni ijumaa mpaka ijumaa. Je ndivyo dini yako inavyoagiza?. 
            Mwingine ni mkristo kwamaana nyingine ni mfuasi wa KRISTO swali je wewe umejifunza kwa kristo kweli mbona haujabeba msalaba wako mwenyewe?. Kama wewe una dini kweli mbona hutuambii mwisho au Taraji ya dini yako kwa matendo tujue u katika safari kweli ya kufika kwenye Taraji ya dini yako. Mtu na akasema mimi niwa Paulo na mwingine mimi niwa Petro na wote wakabaki ni wanadam tu. Je wajua unayemuabudu anataka uweje? Soma sheria zake na usizipindishe hata moja ndipo utajua kuwa mungu wa dini yako anataka nini kwako. Leo hii mtu akisimama kuonya kuna watu wanasema sisi na wewe ni dini moja lakini madhehebu tofauti. Sikiliza nikuambie kila dini iko kwenye Imani ya ibada na ya uwepo wa Mungu. Sasa je kwa mwenendo wa ulimi na matendo yako vinamwabudu bado au umekuwa unaidanganya nafsi yako kila mara?. Sikia nikuambie ndugu kusema wewe ni dini fulani halafu ukaacha baadhi ya sharia na ukaamua kufuata baadhi tu kwasababu wewe umeona ni njema machoni pako mwenyewe. 
            Ama zinakupa uhuru wakutii mambo yaliyo kinyume na hicho unachokiamini. Nasema hivi kwasababu kuna watu wako dhehebu Fulani kwasababu tu hawapendi kuambiwa uzinzi ni dhambi au mavazi yao niya kikahaba. Kwa wakristo Hakuna wokovu pasi na kumpenda YESU na kama ukimpenda Yesu inatakiwa ujikane na ushike sheria zake na uzifuate. Kwahiyo kuwa mkirsto siyo kazi ya lelemama inahitaji kujitoa kwa gharama zote kumfuata yesu. Kuna siku moja mtu mmoja aliniuliza Je BASA wewe kweli umeokoka? Nikamjibu HAPANA  unajua kwanini nilimjibu hivyo???

................................inaendelea bofya hapa kusoma...........


Mwandishi MICHAEL BASA  0765279698

Jumapili, 1 Oktoba 2017

HUYU MUNGU NI BABA

Bwana wewe ni nguvu na ngome kwangu ahadi zako ni za milele kwangu umeniinua juu ya mataifa nawe umekuwa mji wa nguvu moyoni mwangu mataifa sikieni nanyi mkaweke ushuhuda mioyoni mwenu “Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana”. Tena ni “Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake”. Bwana Mungu wangu anawapenda watu hao nao kamwe hawatakuwa makapi mbele za adui zao maana Bwana yeye atawashindia vita na wao milele watakuwa washindi. Je wachamungu wametaabika mioyoni mwao na nyongeza zimeteka ufahamu wao sikieni leo niwakumbushe fadhili za Bwana zilizo za milele tena aliahidi hatakuacha enyi mtangao je hamkusoma imeandikwa “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?. Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”. Je hamkuamini kwa neno la injili nalo ni hili yeye aketiye mahali palipoinuka ametuamru kuyashika mausia yake Ili sisi tuyatii sana. Neno langu naomba kibali mbele zako Bwana nalo ni hili “Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako.Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako”. Kwa maana Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya Injili, akapata hasara bali atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
Inaendeshwa na Blogger.