Jumatatu, 28 Agosti 2017

BASA VISION


 Moja ya mijadala au maswali magum kwa kipindi hiki au kwa wakristo wote ni kwanini shetani anawasumbua?. Nami katika njozi ya usiku wa kuamkia tarehe 28 Aug 2017 Bwana alinionesha. Kwanza siku mbili kabla moyo wangu ulikuwa na kiu ya kitu ambacho sikijui nikaona labda tamaa ya kumtumikia Bwana imekuwa kubwa kuliko jinsi ambavyo naweza kuhimili. Nikaendelea na mienendo yangu ya kawaida ya kila siku huku nikijichunga nisije mtenda Bwana dhambi. Jumapili ya tarehe 27/8/2017 nilipokuwa kanisani nikawa kama amani inaisha kwa kuwa nilihitaji kujua kitu ambacho sijui ni nin?{yaani unaahisi unahitaji kuwa na maarifa fulani ambayo huna lakini mtu akikuuliza maarifa gani huwezi kusema maana hata akili yako haijui moyo unataka nini?}. Amani ikaendelea kupungua mpaka nikawa natamani kuondoka kanisani kuacha ibada nikawa mtu wa mawazo. Nikaamua kuingia kwenye maombi nikanena kwa lugha sikujua hata naomba nini?.Roho alininyima maana yake baada ya mda kule kukosa amani kukapungua kidogo nikaendelea na ibada mpaka mwisho.
   Usiku ndipo Bwana akanionesha katika maono nilikuwa natembea sehem ambayo kuna kisima na bwawa upande mwingine namimi nilikuwa napita katikati yake huku nikiwaza jinsi ya kumtumikia Bwana kwa uaminifu huko niendako?. Kwamaana Bwana alikuwa amenituma lakini sehem siijui, nilipokuwa katika mawazo yale mara mbingu zikafunguka nikamuona Roho mtakatifu akishuka kwa mfano wa hua.  Yesu akasema na mimi akaniambia kuna kanisa hapa nataka ukafundishe ndipo uendelee na safari. Nikakubali nikafunguliwa macho nikaona kanisa ndani ya Yesu mwenyewe nililokuwa natakiwa kwenda kulifundisha nalo lilikuwa na watu wengi sana. 
   Walikuwa wakisifu mbele za Bwana hakika walipendeza sana. Nilipokubali ndani ya moyo wangu mda ule ule Roho alinichukua nikajiona naiacha ardhi na kuingia ndani ya lile kanisa madhabahuni. Waumini wakakaa kimya kila mtu mahali pake ndipo nikafungua biblia nifundishe moja ya masomo ninayoyafaham. Nilipoanza tu kufundisha Roho akaniambia siyo somo hilo tazama huku uwaelezee yote utakayoyaona nami nitakuwa nawewe. Nikaona tazama binti mmoja mlokole aliyekuwa na njaa ya kumtumkia sana Mungu na Mungu akambariki kwa KARAMA ya ualim na huduma ya uimbaji watu wote wakampenda sana kwa jinsi alivyojitoa kwa Bwana. Shetani alijaribu maranyingi sana kumtoa kwa Yesu kwa kumzuia kuimba akashindwa, kwa kumtenga na marafiki, kumkosanisha kanisani hata hakujali walipomkataa kanisani yeye alihudumia wa nje ya kanisa. Watu wakampenda sana kwa nyimbo zake na mafundisho yake mazuri hata Yesu alimpenda pia. Kikao kikafanyika kuzimu kuhusu ufalme wao kutetereka sana kupitia kwa huyu binti wa Yesu. Shetani akaja na mpango mpya ambao angetumia miaka miwili kufikia kumuangusha kabisa na kumtoa nje ya Yesu. Nao mpango ulikuwa katika hatua zifuatazo:-

1. Kuanza kucheza na mawazo yake ya kila siku kuhakikisha  mawazo yake yanaanza kuwa na chembe za uovu kwa mbali kwa vitu vifuatavyo:
  • MWILI WAKE MWENYEWE:- atakapofikria kuhusu nguo za kuvaa kwaajili ya huduma cha kwanza kabisaa ni kumpa wazo la kwamba hizo nguo ni za zamani pia hazimpendezi kwasasa na atakapojiuliza avae nguo gani?. Picha ya kwanza kumletea ni zile za watu waliopotea na bado wanafanya huduma au bado wako kanisani.
  • MARAFIKI:-kuwasogeza marafiki wengi waliopotea kwake wakanisani na wasio wakanisani karibu yake ili pindi akiwaza uovu wao ndio wamshauri uovu ule kwamba hauna madhara kwake kwa maana hata wao bado wanatumiwa na Roho au wanasfari ya kwenda mbinguni
  • MAVAZI:- kuanza kumpa mawazo ya kuvaa nusu uchi na kwa nia ya kupendeza maana huduma siyo ma nguo marefu au mapana sana lakini ni kupendeza kwanza kisha huduma itavutia watu wengi.
  • AKILI YAKE:- ipunguze kuwaza kuhusu Mungu sana au ikiwaza isiwe katika uzito ule wa mwanzo kwa kumpa kitu mbadala cha kuwaza kila anapotaka kufikria kuhusu Mungu.
2. Baada ya hivyo kufanikiwa kinachofuta ni kumpa roho ya kukosa mda kwa maana atapunguza maombi na tamaa ya kuhudumia kwa bidii au kupanda viwango iondoke. 

3. Wazo la mume limjie kwa kasi ya ajabu ambayo mwili wake na akili zake zishindwe kuhimili.. Ambapo iwe rahisi kumpa mtu ambaye atashindwa kufanya jukum la Bwana au kufikia viwango pia iwe rahisi kuingilia ndoa na kila kitu cha ndani ya ndoa. 

4. Kumuacha ahudum huku akiona kila kitu kipo sawa hata asipopotea yeye lakini kazi za ufalme wa giza zitaendelea kuwepo na kukua na kushamiri sana duniani kote.

Baada ya kile kikao nikaona kundi kubwa likimvamia la pepo wachafu kila pepo alitoa wazo ambalo anahisi linaweza kufanikiwa. Baada ya mda mrefu sana hatimae yule binti akaweka mguu mmoja nje ya msitari wa wokovu na nguvu za giza hata bega lake kushoto lilikuwa na alama ya uovu. Mwili wake uliosalia ulikuwa ndani ya Yesu ukipokea baraka zote na kila kitu lakini kuenea kwa ufalme wa Mungu kupitia yeye ilikuwa tayari imekuwa ngumu.

 MICHAEL BASA +255765 279 698 

Alhamisi, 24 Agosti 2017

NUHU WA KIZAZI HIKI

   Ukisoma kitabu cha mwanzo 5:29 mpaka mwanzo 10:32 utakuta habari za mtu mmoja anaitwa NUHU. Huyu mwanaume aliishi katika kizazi kilichokuwa katika hali ya uovu wakupindukia. Watu walilala na wanyama, walikula nyama za watu, walikuwa ni watu wakaidi wasiotii, wasiosamehe,wauaji. Watu walipoona uovu kuwa ni kitu cha kawaida Nuhu alipata kibali machoni pa Bwana. Kama wewe unampenda Mungu kweli utajiuliza ilikuwaje Mungu akamhifadhi katika uovu kiasi kile?. Je unamkumbuka Lutu aliyepata amani machoni pa Bwana pindi moto uliposhuka na kuangamiza sodoma na gomora?. Uovu ulipozoeleka machoni pa wanadam na kuonekana kitu cha kawaida yeye moyo wake ulimwelekea Bwana. 
   Walipoonekana hawana akili na kuitwa wajinga au wasio enenda na wakati kwa wakati huo lakini mioyoni mwao cha kwanza kilikuwa ni kumpendeza Bwana. Unaweza usinielewe haraka kiasi hiki twende pamoja kwenye kitabu cha mathayo 24:36-39 {Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.}. Hata kuja kwake mwana wa adam kwa mara ya pili maisha yatakuwa yanaendelea tu kama kawaida. Kanisa litaendelea kama kawaida, manbii wauongo nao watakuwepo kama kawaida, wachagua wokovu nao watakuwepo, wang'ang'ania kanisa kuliko Yesu nao wataongezeka maana ndiko ukristo unakoelekea. Yesu hajaleta ulokole, usabato, uroma n.k. Lakini alileta uzima wa milele{Yohana 17:3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.}. Tazama leo kuna wokovu wa aina mbili mmoja wa zamani na mwingine wakisasa. Wengine wameanza kuchagua maandiko ya kwenye wokovu wakisasa. 
   Ukimkemea anajenga chuki nawewe hata anaweza kutengeneza somo kwaajili yako tu je huyo Roho anayewapa amani ni kweli ndiyo huyu ninayemtumikia mimi?. Kwamaana kuna wengine mioyo yao ndio waalim wao hata wamemzimisha Roho mtakatifu kasome tena Yeremia 17:9, Yakobo 1:22b na 1Wathesalonike 5:19. Kuna kanisa moja Mungu aliniweka niabudu hapo nikakuta ibada zao ni kusemana baada ya kukosekana nikaazimu moyoni mwangu kulihama ili nikatafute kanisa jingine. Bwana akaniambia hapo ndipo nilipokupangia uabudu. Ikawa ni mtihani kwangu katika wokovu wakuanza kuwatoa watu huko kwenye mafundisho yakusemana na kuja kwenye mafundisho yakutiana moyo na kujengana katika mwili wa Kristo pia msamaha mioyoni mwao. 
   Nilikuwa naongea na mmoja mmoja kisha nikaongea na kundi zima kama Bwana alivyonipa neema na kibali pia. Lakini pia kuna mtu Roho alinishuhudia nikamwambie kuhusu mavazi yake ayabadilishe ili roho{nguvu} ya uasherati isimsumbue tena au imuache. Alikuwa ameokoka akaniambia kuwa hicho ninachomwambia ni wokovu wa zamani sana. Lakini baada ya mazungumzo marefu na kujitahidi kujibu maswali yake akaniambia baadaye atafikria kuhusu kubadili mavazi yake. Lakini haijalishi kuwa kuna wokovu wa zamani na wakisasa lakini sikia nikuambie kuwa {HAIJALISHI DHAMBI WANAFANYA WENGI KIASI GANI?, AU IMEZOELEKA KIASI GANI?, AU WANAFANYA WATU UNAOWAAMINI KIASI GANI LAKINI DHAMBI ITABAKI DHAMBI  SIKU ZOTE NA ITAKUFANYA USIENDE MBINGUNI?}. Mungu wetu ni mtakatifu na mtakatifu pekee ndio atamuona yeye na ndie atakayepata ruhusa ya kuingia kwenye makazi yake. 
itaendelea........
MICHAEL BASA 0765279698

Ijumaa, 18 Agosti 2017

JE NI MIMI au NI BWANA??.

Kuna kipindi mkanganyiko hutokea sana pindi tu linapokuja suala la mipaka ya Bwana kutenda na wewe mwenyewe kutenda. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema nanukuu " usiufiche uzembe au uvivu wako kwenye maombi ukahisi utafanikiwa bali fanya kazi kwa bidii Bwana atakutana nawewe huko huko kazini". Pia kuna mwingine aliwahi kusema kwa kiingereza "hard work beats talent when talent doesn't work hard". Lakini biblia inaseema "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu." katika wafilipi 4:6. Swali la kujiuliza je kuna mipaka ipi ya kimwili na kiMungu katika utendaji wangu yaani ya kimwili na Roho katika uenendaji wangu wa kila siku?. Kabla ya kujibu hili swali tuangalie kwanza andiko moja nalo ni kutoka wagalatia 5:25 "Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.". Kuna vitu vifuatavyo katika kuishi katika mwili huku ukifanya ya rohoni navyo ni:-

  1. Katika mtazamo wa kwenda mbinguni au kuingia Yerusalem mpya inatakiwa uwe kwanza akilini mwako kila mahali unapotembea au kukaa au hata kulala. Kwamaana mshitaki yuko kila mda anaandaa hati yako ya mashitaka nawewe uwe katika hali ya kuvunja shitaka shitaka lolote litakaloletwa{1ptero 5:8}. Hapo cha kwanza ni kujazwa ROHO mtakatifu na kumsikiliza yeye tu kama mwalim, msahuri, mwelekezi wako, mtoa dira wako, mpangaji wa mambo yako yote, msemaji wa mwisho juu yako na rafiki bora kwako.warumi 8:9 pia yoha 14:26.
  2. Jizoeze kuwa mkazi wa mbinguni kwa kujifunza mambo ya ufalme na kujizoeza katika mambo ya ufalme kila mara.  1Petero 2:11 "Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.". Wewe ni msafiri tu usitake kuupata ulimwengu kwanza bali tunza kwanza taji ufunuo 3:11, marko 8:36. Safari ya mbinguni iwe ni ya uhakika maishani mwako mwote.
  3. Acha kuishi kwa mazoea kila siku Mungu anataka kusema na wewe kwa jinsi nyingine na tofauti sana kutoka ile ya jana. Usimzoee Mungu kwa maana ukiona umemzoea sana Mungu jua tu umeshaanguka. Kwamaana mda si mrefu ulishapingana na Roho mtakatifu. Kuna watu wamekariri jinsi moja tu ya kusema na Mungu jua kwamba safari yako haina uhakika sana kwa maana hata shetani anaweza kutumia na akakupoteza na Mungu akatumia njia nyingine ukashindwa kumuelewa kuwa ni YEYE anayesema nawewe. Penda kuona Mungu akijifunua kivingine kila siku katika maisha yako ya kila siku.
  4. Penda sana kujihoji uhusiano wako wa siku kati yako na ROHO kwa maana unaweza kutana na ishu ngumu au hali ambayo akili yako ikashindwa kutafasiri kwa jinsi ambavyo Mungu anapenda au anataka uelewe. Ukijihoji atakuambia na kukuelekeza kisha unatubu mambo yanakuwa sawia kabisaa.
Baada ya kuanza kutenda hivyo vinne utakuja kugundua kwamba roho yako inaanza kuwa na nguvu sana kuliko mwili wako. Hapo ndipo unakuwa na uwezo wa kuongea na Mungu bila wasiwasi na kuishi kwa imani unakuwa mtu wa mfano  kwa jamii yote katika imani. Ukiwa mtu huyo hauhitaji unabii wala nabii akuambie Mungu anasema nini juu yako kwamaana kabla hujaja hapo ulipo tayari kashasema nawewe. Kama ndivyo hivyoo basi mtendaji ni wewe na Muongozaji{mwamuzi} ni Bwana na nyie wawili mnakuwa umoja kwamaana mnaishi ndani ya jumba moja ambalo ni mwili huo ulio nao na nyie  mmenakuwa mmoja. Na hapo  ndipo kila ufanyalo litafanikiwa kwamaana Mungu anakuwa anataka akutumie sana. Kwahiyo hawezi kuruhusu upoteze mda kwenye mambo yasiyokuwa ya ufalme wake. Kila utakapofanya swali kubwa litakuwa JE NI MIMI au NI BWANA?. Jibu ni Bwana ndani yako kwa nje unaonekana wewe kwa ndani anaonekana Bwana. Ndipo hata mtu akikushukuru haujitukuzi kwamaana ile shukrani ikiingia ndani inamkuta Bwana kila sehem na Yeye ndiye anayeipokea. 
   Mungu akubariki sana mtumishi  kwa kusoma mpaka mwisho tumia namba yangu hapo chini kunipa mrejesho na pia kutoa maoni yako. Pia nataka nisikie kutoka kwako na kwa facebook page usiache ku LIKE 

By MICHAEL BASA +255 765 279 698

Jumanne, 15 Agosti 2017

NANI ASIMAME AKEMEE ???.


 Nami nimeuona uovu juu ya madhabahu maana dhambi ya kipindi kanisa linakuja kwasasa haikemewi tena. Nani kasema kuwa Yesu kabadilika au sheria zimetanguka, kama mwanzo tulikemea kunyoa DENGE na tukaamini kuwa ni uhuni na pia haufai kanisani leo kimetokea nini isiwe dhambi tena?. Soma walawi 19:27 {You shall not round the corners of the hair of your heads nor trim the corners of your beard [as some idolaters do] kutoka kwenye AMP}.  Hiyo style ya kunyoa ya denge ilikuwa inatumiwa na waabudu sanam na pia tatuu inatumiwa na waabudu sanam kama alama ya kujisogeza kwnye ibada.Mfano kwenye makanisa ya sasa tunatumia nyimbo za kuabudu ili kujiweka tayari mbele za Mungu. Sasa wewe unayenyoa au unayetamani ujichore tatuu je unajua kwamba mawazo yako yameanza kukutoa kwenye kumwabudu au kumtumikia Mungu wa kweli nakuanza kuielekea miungu ambayo haitakupeleka mbinguni bali kuzimu. 
     Tazama tena kwa mabinti zetu nguo walizovaa makahaba miaka 1970 leo ndio zinavaliwa na waimbaji wa makanisa yetu . Mtoto wa mchungaji akifanya dhambi ni nani wa kukemea huo uasi. Sikia mbinguni hatuingii kwa vyeo vyetu ndani ya kanisa wala huduma zetu ndani ya kanisa hakika nakuambia BASA MINISTRY haitanipeleka mbinguni bali UTAKATIFU ndio utanipa kibali cha kukutana na Bwana wangu. Waumini wameanza kuchagua mafundisho ya kushika wakati biblia ni moja wewe usiye na akili ni nani aliye kuroga wainjilisti wamesema wazi na kukemea wazi mbele zako nawewe ukainua kimdomo chako kumsema vibaya pole sana. Kwamaana wafanya vita na Bwana mwenyewe nawe hutaokoka kwa mawazo yako maovu wala kujihesabia haki kwako. 
   Ni nani kati ya mabinti zetu aliyetaka kununua kimini akaammua kufunga na kuomba kwaajili ya kupata maono na ruhusa ya Roho mtakatifu na baada ya kupata jibu akashirikisha mwingine zaidi kwenye kuomba maono kuwa Roho analionaje hilo vazi?. Vijana wa kanisa nao hawako nyuma kwa msemo wa modo zao nguo inabana kila sehem. Mwanzo wanawake walivaa kuamsha hisia{lust} za wanaume je kijana wa kiume unaamsha hisia za nani?. Je unajua madhara ya kutumika kwenye kitu ambacho mwanzilishi{author} wake siyo Mungu?. 
    Nakuambia acha kuiga iga vitu ovyo tamani kwanza kujazwa Roho mtakatifu kisha ipeleke injili kwa jinsi ulivyoitwa tamaa za mwili huwezi kuzikamilisha milele mpenzi wangu nikupendaye na pia shetani ni mdanganyifu sana wewe jisifu kwa Amani yenye mapengo mapengo na roho yako mwenyewe imechoka na haiwezi kumuona MUNGU. 

By MICHAEL BASA 0765 279 698

Jumapili, 13 Agosti 2017

UNAWAZA NINI??

unawaza nini
basa jpg
    Kabla ya kitu chochote kudhihirika kwenye ulimwengu wa mwili kiutendaji huanza kama wazo ndani ya moyo au akili ya mtu mwenyewe. Kwa wazo lako  unaweza kuanzisha vita ya kiroho au kujisogeza karibu zaidi na MUNGU wako. Mwanzo 4:7 inasema ........dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Angalia kwenye hayo maandishi mekundu utajua kitu tofauti kidogo. Dhambi iko inakuotea mlangoni???? jiulize tena kivipi dhambi ikuvizie mlangoni kwako. Lakini pia inakutamani!!!! kivipi haya yanawezekana kutoka kinywani mwa MUNGU mwenyewe. Kama wewe ni mchunguzaji wa maandiko huenda na wewe ilikutatiza sana au kiasi chake.
       Twende zaburi 36:1{Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.}au Ezekieli 38:10. Kumbe kabla ya mtu kutenda uovu machoni  pake huja na wazo moyoni mwake likipita ndilo hulitenda bila kuwa na hofu ya Mungu kabisaa. Basi kumbe dhambi haiwi dhambi mpaka ipate kibali moyoni mwako. Usipoipa kibali kamwe wewe hauwezi kutenda dhambi kabisaa katika maisha yako yote. Jikune kichwa kidogo kisha jiulize asilimia kubwa ya mawazo unayowaza je niya ufalme upi??. 
      Soma tena zaburi 66:18 {Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia}. Swali la kujiuliza je ni Bwana hawasikii watu gani?    Yeremia11:11-17 hapa ndipo utagundua kuwa walioasi au kuiacha sharia ya Mungu ndio ambao Bwana hawasikii. Daudi anaposema Bwana asingesikia basi kwa namna moja au nyingine anakukumbusha kuwa dhambi huanzia moyoni mwa mtu. Huhesabiwa kuwa ni dhambi baada ya kupata kibali moyoni mwako mwenyewe ndio maana katika Yakobo 4:1. Imeelezea kabisa kuw vita tunavyopigana mara nyingi kwa kushindana na miili au viungo vyetu zimetokana na mawazo yetu yasiyo na kibali machoni pa Bwana. 
          Ndio maana YESU akatuonya mapema kwa kutuelekeza kuyatafakri yaliyo juu yapitayo faham zetu. Leo pia nakukumbusha usikomee kuwaza tu mazingira yako hayo yatakukatisha tamaa MUNGU haangalii mazingira wala jamii ya watu waliokuzunguka. Kwamaana hata hao hawajui Mungu anakuwazia nini? bali watasema yajazayo mioyo yao kama  mawazo yao ni maovu . Basi hata mioyo yao huwa imejaa maneno na shuhuda za kutomtukuza Bwana wala kuonesha ukuu wake hata zikikiri kuwa ni muweza wa yote lakini bado huwategemea wanadam maana mioyo yao huwa imeielekea zaidi dunia na siyo ufalme wa Mungu. Yeremia29:11 na akaambiwa asijisumbue wanasema nini juu yake kwa maana hawajui Bwana aliwazalo wala alipangalo juu yako pia  MIKA4:12. 

By Michael Basa 0765 279 698

Alhamisi, 3 Agosti 2017

KANISA LILILOPOTEA--2

      Kuna jinsi mbili za ambazo shetani hututmia kumtawala mtu mosi ni njia ya moja kwa moja. Katika hii njia mtu anakuwa anajuwa kuwa mimi ni washetani na hata sasa nikifa mimi nitaenda kuzimu lakini kwa sababu ya mambo fulani fulani siwezi kutoka huku mfano waabudu sanamu, wachawi n.k. Pili ni njia isiyo ya moja kwa moja hili kundi limegawanyika sehem mbili ya kwanza ni ile ambayo haiombi kabisa kwa MUNGU. na ya pili ni ile ambayo inaomba kwa MUNGU. Makundi yote unakuta yanamilikiwa na shetani pasipo na wao wahusika kujua. Watu katika kundi hili unaweza kuta mpaka ni viongozi wa kanisa lakini bado matendo ya mwili ni dhahiri kwao. Je hujawahi kukuta shehe kalawiti mtoto?.
         Je RC nayo amabayo watu wanaipigia kelele rome kila siku watoto wanaingiliwa kinyume na maumbile. Monoroviani ambao nao katika nchi za UK wameruhusu mashoga kufunga ndoa tena wanatumia biblia??. Je unafuu uko wapi PENTEKOSTE nako ambako ndoa zinafungwa huku binti tayari anamimba??. EAGT na TAG ambako mzee wa kanisa anakimada ndani ya kanisa lile lile?. Wamama wa makanisani nao wamejaa maseng'enyo unaachaje kusema hili ni kundi ambalo baya zaidi kuliko lile la kwanza. kwamaana hili ni kundi linaloodhifisha na kupoteza kanisa kuliko la wachawi na waabudu sanamu wala wajenzi huru.
          Kwamaana watu wengi wanashindwa kumfuata YESU katika ROHO na kweli kwasababu yenu ninyi viongozi na wachungaji vipofu. Injili zenu zimebaki kukemea wenzenu wa mafundisho fulani au waaina fulani tu. Mfano mzuri ni huu msitari waefeso 2:20{Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.}. Msingi wa kanisa lako umejengwa juu ya akina nani kama mafundisho yako wewe ni juu ya manabii tu na siyo kufundisha jinsi ya  kutofautisha nabii wa uongo na nabii wa ukweli?.
          Kuna mchungaji unamkuta mafundisho yake yote yanaongelea mafundhisha ya manabii wa uongo tu basi hebu anza kuliangalia hili andiko pia 1yohana 4:1{Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.}. Hebu anza kufundisha kanisa lako kutembea katika Roho uone kama atapotea hata mmoja kweli kwa maana umewafanya kila waumin wako kila siku kuwa ni watoto wadogo wakati kwenye kanisa lako ambalo halizidi hata huduma tatu. Na umekaa kimya tu na kuridhika kabisa je huduma zingine za ndani ya kanisa umeziweka wapi kama siyo kwamba umezikataa mwenyewe tu??.
        Naomba kwako leo ewe Mchungaji au Padri hebu jaribu kufufua karama zote na wafanye watu watembee katika Roho ndipo utaona ni kwanini watu wanahitaji kweli tu uongo utajitenga wenyewe. Pia naomba nieleweke kuwa sijakataa kuwa manabii wa uongo hawapo bali na makristo wa uongo wapo tena wengi kuliko hata manabii. Je kuna nyimbo ngapi za injili hazina utukufu katika uchezaji wake au uimbaji wake na hazimjengi mtu katika imani?. Basi kasome tena utakutwa imeandikwa katika 2wakorintho 1:21 {kuna mtia mafuta mmoja ambaye ni MUNGU} kisha kasome 1Yohana2:20-28 utajua ni kwanini natamani ujae ROHO Mtakatifu hata hutasumbuka na kuchukia mafundisho wala wafundishao bali utajua kusudi lako ni nini juu yao. Pia kuna roho ya ibilisi imekaribia kuanza kuingia makanisani na itakuwa na nguvu sana nayo ni KUJICHORA{TATTOO} nakuonya mapema anza kuikemea sasa na kufundisha kuwa kujichora ni dhambi na mtu akijichora atengwe kabisaa bila kujali cheo chake wala karama yake usije, nimekuonya mapema wewe na kundi lako.
     by MICHAEL BASA 0765 279 698
Inaendeshwa na Blogger.