Jumapili, 30 Julai 2017

KANISA LILOPOTEA

 
   Makanisa ni sehem nzuri sana ya kusanyiko kuonyana, kuelekezana, kufundishana na kutiana moyo katika njia ya BWANA. Lakini kanisa hilo pia linaweza kupotoka na kuacha kuweka mkazo kwa washirika kwenye safari ya kwenda mbinguni na kurukia mambo ya kidunia. Kuna makanisa yanapinga injili za kufanikiwa sijui wanatumia biblia gani?? Hebu soma torati 28:1-22 lakini rudia tena kuusoma msitari wa  12{hasa hapa………nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.} fikria kwa kina huu msitari. Je ulishawahi kumuuliza ROHO mtakatifu kuhusu kanisa lako juu ya huu msitari. Naye alikujibu nini?? Je alikujibu kuwa na mali ni anasa na je matajiri wote hawataenda mbinguni??
       2wakorintho 8:9 { Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.}. je huu nao haupo kwenye biblia yako mtumishi wa MUNGU aliye juu??. Haijalishi wewe ni nabii au mwinjilisti kwangu hakuna tofauti kwamaana biblia yasema kila mtu na atuhesabu hivi tu watenda kazi pamoja na KRISTO. 
         Lakini katika kutenda kazi pamoja na KRISTO kumbuka kumtumia ROHO wake ili kutengeneza mambo yaliyopo na yajayo kwa usahihi zaidi. Kwamaana watu makanisa yameacha injili kamili ya KRISTO na kujikita kwenye magomvi ambayo yanamuudhi ROHO wa BWANA na kumpa ibilisi utukufu. Na kuna mmoja ambaye alianza katika ROHO naye kamalizia katika mwili. Kaligawa kanisa kati ya wallio nacho na wasiokuwa nacho.
        Ewe mwana wa laana ni nani aliyekupa ruhusa ya kugawa mafungu watu wa aliye juu kwa tamaa zako mwenyewe. Basi BWANA amekutaa wewe na wana wako na nyumba yako omboleza kwa tumbo na kwa utungu anza sasa. Lia wewe uliye nyamaza naamu kesha mavumbini hata asubuhi maana BWANA hatakuacha salama.
          Kuna mwingine aliyepotea yeye na kanisa lake lote hata dhambi imekuwa kitu cha kawaida kanisani. Mchungaji anatafuta injili ya kutafuta watu waongezeke lakini hawapi nafasi ya kukutana na kumjua ROHO MTAKATIFU. Hii siyo injili ambayo YESU aliitaka ihubiriwe na watu wake ni injili ambayo cha kwanza kitakuwa ni kuingia YERUSALEM MPYA na siyo kuimiliki dunia.
By MICHAEL BASA 0765279698

SHULE YANGU NDANI YA YESU


  Elimu ni bahari aka haina mwisho wahenga walisema. Tunajifunza kwaajili ya kupata uwezo wa kufikria zaidi ya hapo mwanzo au Kufikria kwa jinsi bora zaidi. Kuliko ile ya mwanzo tuliyokuwa tunaitumia. Kuna kipindi mwanadam  uwezo wake wa kufikri hukoma na huhitaji kupata maarifa au elim zaidi ili aweze kuenenda sambamba na tatizo lake kufikia utatuzi. Kuna maarifa ya safari ya kuwa mkazi wa  mbinguni.
    Haijalishi uko kanisa gani wala kanisa lako lina historia gani tokea kuanzishwa kwake. Kuna watu wanasifia sana wachungaji wao kuwa ni manabii au wanaupako sana kuliko wa kanisa fulani; lakini huo uasherati wako ndio utakaokufikisha mbinguni?????. Hebu fikria tena hayo mavazi yako ya nusu unayovaa kwa kigezo cha kupendeza je ni upako wa mchungaji wako au ni historia ya kanisa lako ndilo limekuelekeza hivyo??. Kuna watu wanajisifia kuwa wameokoka na wameona kuwa ni sifa kuokoka au ni jambo la kutumainiwa sana lakini je huo uongo wako nao ni moja ya wokovu?.
   Unaijua kweli gharama ya kufika mbinguni au kusoma kozi ya mkazi wa mbinguni na kuifaulu kweli wewe??. Subiri ni kuambie kitu ukitaka kujisifu na ujisifu katika KRISTO{2wakorintho10:17}. Faulu kwanza masomo ya ROHO MTAKATIFU amabaye anafundisha masomo sita nayo ni 1}KUUSHINDA MWILI 2}KUSHIKA NENO LA BWANA 3} MAOMBI 4} MIFUNGO 5} KUMTII BWANA na  6}UTAUWA. Hizo ni kozi ambazo ni lazima ufaulu na hapo hakuna kozi ambazo tunajisifia sana huku kwetu kama 1}KANISA LETU TUNASOMA SANA BIBLIA 2}KANISA LETU LINA HISTORIA KUBWA 3} MIMI NIMEOKOKA WEWE HUJAZALIWA 4}DINI YETU INAAMINI KWENYE KULA NA SIKU 5} MUNGU WA ELIYA NDIYO MUNGU.
     Hizo zote ni porojo tu za hapa duniani naza watu waliopotea sana. Je hujawahi kuona watu wa  mataifa ambao nafsi zao zinashuhudia ndani yao kuwa wamepotea wanakuhukum wewe na bado wakajihesabu wao ni bora kwako hata maramia. Ndio  maana nasema rudi SHULE YA YESU ukajifunze tena kwake kwamda zaidi. Ndipo utajua kuwa ni kwanini mmoja wa wanafunzi alifurahia mateso na kuhesabu kila kitu kuwa hakina thamani tena?. Au ni kwanini YESU alisema kuwa mtu akimpenda ndugu yake au mwenza wake kuliko YEYE hafai kuwa mkazi wa mbinguni??. Chagua leo kurudi miguuni pa MUNGU  ukajifunze tena upyaa ndipo matunda yataonekana waziwazi na watu watakiri kuwa wewe ni mmoja wa wakazi wa mbinguni.
                      by MICHAEL BASA +255(0)765 279 698
Inaendeshwa na Blogger.