Jumatatu, 10 Aprili 2017

UKITAKA NISIWE HAPA FANYA HAYA

 
         Nilikuwa nafikria mfano wa kwamba kama majira ya kuzaliwa YESU asingekuwepo bikra je angezaliwa au angesubiria?. Ndipo nikagundua kwamba utakatifu wa MARIA ulikuwa ni sifa ya kumtofautisha kutoka kwa mabikra wengine wa kipindi hicho. MUNGU hujisazia watu anaowataka yeye mwenyewe kwa kazi yake maalum na shetani anapewa ruhusa tu ya kumgusa yeye na siyo kugusa kile kinachobeba utukufu wa MUNGU. 
             Ukitaka kujua kwanini upo unaishi mpaka leo tafuta kujua kususdi lako la kuzaliwa sio la kuishi. Kuna tofauti kati ya kuzaliwa kwa kusudi na kuishi kwa kusudi. Kuzaliwa ni hatua ya kuwekwa kwenye mazingira ya kufanyia kazi yako{To be born is the chance of a new man to be exposed to a working field}. Lakni kuishi ni kipindi cha kufanya kazi yako uliyopewa. Ndio maana unaweza kuacha kufanya kazi uliyopewa kwenye mazingira uliyowekwa na bado ukaishi. Kuacha kutumikia kusudi halisi inasababishwa na mambo matatu makuu nayo ni:-

  1. KUHARIBIWA KWA WAZAZI WAKO: kwa kawaida mtu huzaliwa hajui chochote maarifa yote huyakuta duniani. Lakini yeye mwenyewe anakuwa hana uwezo wa kutofautisha chochote mpaka ajifunze. Nayo huchukua mda kujifunza na baadaaye huamua nini ashike na nini asishike. Ndio maana mtu aliyepata nafasi ya kuishi na watu wengi tofauti anakuwa na uwezo wa kufkria zaidi kuliko yule ambaye hajapata huo wasaa. Wazazi wa mtoto ndio humfanya mtoto achague ujenzi wa msingi wa mtoto wao baada ya kuzaliwa. Wazazi ukitaka wanawaza tofauti na kile cha ndani yako ambacho MUNGU amekupa kwaajili ya watu wengine. Hakika utakufa nacho kikiwa bado hujawahi hata kukitumia kabisa. Wazazi wengi kwa ufaham wao wanajua kuwa mtoto akisoma ataajiriwa na kisha maisha yake yatakuwa mazuri tu. Na mtoto anakua anajua hivyoo kwasababu kafundisshwa hivyoo. 
  2. MAZINGIRA YASIYO RAFIKI:- Mtu anakulia kwenye mazingira yasiyo rafiki kabisaa. Pata picha kwa hicho unachokifanya je nichako mwenyewe au ulikiona kwa mtu kafanya au hata hujui kwanini unakifanya?. Kuna watu ni waanzilishi wa vitu kutokea na kuna watu niwaendelezaji tu. Ukikuta anayetakiwa kuanzisha anawekwa kwenye mazingira ya kuendeleza basi hakuna atakachoanzisha maisha yake yote.
  3. KUHARIBIWA KWA UWEZO WA KUFIKRI:- Kuna mifano mingi sana kwenye huu upande kuna watu wapo na kila kitu cha kuonesha karama zao lakini wameshindwa aidha hawajiamini au hawaoni umuhimu wa kuwa mtu maarufu kwa karama hiyo. Kuna wamezaliwa kuongoza na watu wa kuwatia moyo wapo na pengine watu wakuwaunga mkono wapo. Lakini hawapendi kuongoza lakini kwenye mkumbo wa kulalamikia uongozi wamo. Ukichunguza unakuta uwezo wao wakufikria kiuongozi hawana kabisa hili ni tatizo kubwa sana.
BASA asingekuwepo leo BASA ministry isingekuwepo. Kuna mda MUNGU huamua kutumia mazingira magumu{harsh condition} kwaajili yako wewe kuonesha uwezo alioweka ndani yako. Ngapi umejaribu kuwa mtu asiye wewe na umeshindwa hebu rudi Mungu anataka kukufundisha na kukuelekeza wewe ni nani na uanze kufikria vipi?. Once you fail to be who you are?. Soon you will be the enemy of yourself and prey of your opportunities. Live in JESUS and become who you are.  

Jumamosi, 8 Aprili 2017

FEEL LOVED

Napenda kupendwa na ninapenda kupenda pia nafurahia kila kitu katika maisha yangu kwasababu nakipenda kukifanya na kinanipa amani katika matokeo yake. Nampenda YESU maana yeye alinipenda kwanza mpaka akatoa uhai wake kwaajili YANGU. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake{yoh 15:13}. Bibilia ilinishangaza sana kuniita rafiki wa YESU kwamaana hatakuja kunificha kile anachofanya kwaajili yangu wala anachowaza hata yale mafumbo ya siri kanipa akili ya kuyajua{yohana 15:13-17}.
             Wakati kuna watu wanamiungu yao wanamitume wao wanawaalim wao na haawajawahi kuwa marafiki nao hata hawakuweza kutolala kwaajili yao{yohana 8:31-35}. Lakini mimi nimekarimiwa pendo lipitalo mapendo yote namimi kubaki na agizo la kushika maagizo tu. Namjua yeye ni pendo na yuko karibu nami kuliko watu wote wala hapana mtumwa, wala ndugu ajuaye siri zangu kuliko yeye.
           Kanipeleka angali ni mchana kutenda yaliyofichika kwenye hekima za wanadam wenye busara na vichwa vyenye mvi{yohana 12:35}. Naam pendo limenikirimia ujasiri wa kuingia patakatifu pa patakatifu pake bila mbuzi wakutekezwa mkononi wala kafara ya kutekezwa wala kujihesabia hatia. Nikapewa mamlaka juu ya mapepo na yule mkuu wa anga la giza akawekwa chini yangu {mathayo 10:19}. Huku ndiko kutawala kwa mwanzo mwanadam alikopewa edeni. Pia pendo hili limenifanya mfalme na kuhani pia. Likanipa pia nguvu yakushinda kila kushindana kutakapo kuja kwenye njia ya BWANA wangu.
                    Nimejipumzisha kwenye hili pendo na uzuri wake umenipa amani na furaha navyo havitakishwa kesho maana tumaini lipo mbele yangu siku zote za maisha yangu. Nafurahia kupendwa nami nampenda pia tena ROHO wake amenipa ili kuwa mwana wake nami nipo kwenye pendo la MWANA wake.Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake{yohana 15:10}. Hata aliye mkuu asiyekuwa kwenye hili pendo ameshushwa hata chini kupita kuzimu. Naam mpumbavu yupo aliyemkubali BABA na kumkataa MWANA amekuwa mpumbavu kuliko wengine wote kutoka kwenye tumbo la mwanamke. Kulikataa pendo liloshushwa na BABA ni sawa na  kuiona njia ya kuingia uzimani na ukajikwaa katikati yake na kuanguka hata usiweze kuinuka.
           Namwingine ni yule aliyejiambia nafsini mwake hakuna MUNGU amekuwa sawa na makapi yapeperushwayo na upepo usiokuwa na hijara huko uendako . Nimejipa neno la maarifa hata limekuwa la kuaminiwa na mataifa pendo husitiri udhaifu wangu kila siku hata sasa nimekuwa kamili katika mambo yote. Aabuduye miungu na ajipepeleze nafsini mwake kwa kazi ya mkono wa mwanadam ameifanya tumaini lake je si mtu asiye na akili tu awezaye kufanya hivyo?.
               Nami nilipopungukiwa na akili nikayumbishwa huku na huko kama merikebu katikati ya bahari iliyojaa taabu ni sawa na siku ya utungu wa mwanamke mpaka nilipogundua kumtumikia BWANA pekee. Pendo lake limefuta machozi hata sasa ni mwana wake kweli ampendezaye babaye na BABA kamkirimia pendo lipitalo mapendo yote. Hata amani amenipa ambayo ulimwengu huu hauwezi kunipa. Ninatumaini la maisha ya sasa  nayajayo kwenye ulimwengu huu na ulimwengu ujao. wangu Kila kunapokucha na kutafakari ukuu wa BWANA.
    I SMILE AND SAY '' I FEEL LOVED''  
Inaendeshwa na Blogger.