Jumanne, 28 Machi 2017

SOMO:- AINA ZA UVIVU

Kuna aina tatu za mtu mvivu kibiblia nazo ni
1.                       MVIVU WA KUTOANZA KUFANYA JAMBO:- huu ni uvivu namba moja kwangu kwa maana kwa mtu mvivu kwake ni kitu cha maana kabisaa kuja na sababu ya kuacha kufanya kitu Fulani pasi na kuangalia sababu za kufanya hilo jambo. Huwa ni mzuri katika mifano ya kushindwa na mitazamo ya kutofanikiwa kuliko kufanikiwa kwake. Mtu mvivu anaweza kuamua kuanza kufanya biashara bali akafikiria kisha akamfikiria mtu mmoja aliyeshindwa kuimudu hiyo bisahara kuliko watu kumi wanaofanya kwa mda huo na wamefanikiwa. Kwa huyu mtu kila changamoto kwake ni kamba ya kumrudisha nyuma kuliko kupambana. Kwa huyu mtu ni ngumu sana kuuona mkono wa MUNGU ukitenda kwake. Mithali 6:9 na mithali 26:13-14
2.                           
 MVIVU WA KUTOMALIZIA JAMBO:- hebu fikria mtu ambaye anaamua kuanza kula. Anaanza kupika mpaka anamaliza anaweka mezani ananawa na mikono halafu anajihisi uvivu kula. Huu ndio uvivu ninaouongelea hapa. Uvivu wa hapa huwa waajabu sana na watu wengi huwa unatukuta.
                 Mfano wa kawaida unaamua kuanza kufanya jambo Fulani na maandalizi yake unayakamilisha halafu kulikamilisha unashindwa au unakata tamaa. ‘Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.’’{mitha 19:24}.  Uvivu wa jinsi hii humfanya mtu asione mafanikio ya kila  anachofanya. Pia hushindwa kupanua hozi yake na mafanikio yake huhesabiwa kwa leo tu wala si kwa kesho na motto wake ni ngumu kurithi kutoka katika uvivu wa namna hii.
3.                           
   MVIVU ALIYEKOSA MAARIFA:- aina hii ya uvivu ni maarufu kuliko mwingine wowote. Maana mtu hutumika katika huu uvivu pasi na kujua. Huu huja katika sura mbili nazo ni 1) kufanya jambo tofauti na mipango ya MUNGU juu yako.
                Mungu anaweza kuwa ameweka Baraka zako shambani nawewe upo mjini basi wewe unahesabiwa kuwa ni mvivu katika ulimwengu wa roho. 2)ni mtu ambaye yuko sehem sahihi ya kupokelea Baraka zake. Lakini kumbuka Baraka hazipo kama mvua nyikani bali zipo kwenye kila ufanyalo na yeye akakaa ila kufanya jambo basi atakuwa masikini. ‘’Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu’’{mitahali 20:4}. Huyu mvivu anayeongelewa hapa ni yule ambaye majira sahihi ya kufanya jambo anakuwa hataki kulifanya hilo jambo. Majira yakipita ndio hugeuka kuja kulifanya ndio maana biblia ikasema ‘’hataki kulima wakati wa’’. Ingekuwa hataki kulima majira  yote isingesema wakati wa……
Basi ndugu katika BWANA anza kuomba sasa uvivu wa aina yoyote ukuepuke kabisaa. Maana MUNGU anataka kukubadilisha wewe na kila kitu chako kutoka mhitaji mpaka asiye na uhitaji. 
Mwandishi :- MICHAEL BASA

Jumanne, 21 Machi 2017

BARAKA ZAKO ZIKUJIAPO

MUNGU ni mfano wa mwanadam uliojificha wenye sifa na maamuzi na hisia kama mwanadam uliozungukwa nautukufu pande zote. Tofauti kubwa kati ya mwanadam na MUNGU ni ibada na dhambi. Mwanadam hutafuta kitu chenye uwezo mkubwa na kukipa sifa ya MUNGU{maana mungu ni cheo tu na siyo jina ni kama kusema raisi hi hutegemea na nchi yako na mtu aliyepo madarakani na siyo mtu fulani} na chenyewe hakiwezi kukipeleka hiyo sifa sehem nyingine. Ndio maana mwanadam humwabudu mungu na wala mungu hamwabudu mwanadam. Ukikuta mungu ana mungu wake kuna sifa ya kiungu hupungua kwake mfano mungumtu. Basi ukikuta mungu wako ana mungu mwingine ujue huyo yupo kwa kazi fulani na kuna anashindwa kutenda mpaka umjue mungu mkuu wake maana yeye ndio anampa mungu wako nguvu za kujibu  maombi yako. Kingine ni dhambi, haya ni matendo au fikra ambazo mungu unayemtumikia anazipinga kwenye ufalme wake au kwenye ibada zake. Mfano wake ni MUNGU-YESU kutamani uasherati na mfanya uasherati wote ni wamefanya zinaa katika ullimwengu wake. Basi tujikite kwa MUNGU muumba mbingu na nchi na aliyeandikwa kwenye biblia tu maana sitajikita kwa miungu wengine waliobaki nje ya huyo.
        Baraka ni mafuta au nguvu anayopokea mtu kwaajili ya kumiliki kitu vitu au eneo pamoja na vilivyomo ndani yake. Basi MUNGU akikubariki kwenye kazi fulani amekupa kila kitu kinachohusiana na hiyo kazi kinachobaki ni wewe tu kujua nguvu ipi itumike wakati gani?. Mfano mzuri maarifa yapi yatumike wapi na kwa wakati gani?, busara itumike kwa mtu gani na kwanini??, watu wa jinsi fulani uwamiliki vp?, pia nguvu ya maono ya kazi unayofanya utaweza kujua kipi ni muhimu kwa majira  na nyakati zake. Lakini ili MUNGU akubariki inakubidi ujitahidi kugusa moyo wake maana bila hivyo huwezi kufanikiwa katika baraka atakayoiachia kwako. Ukisoma torati 28 utakuta baraka nyingi sana ameahidi MUNGU kukupa lakini baraka zote hizo zimegeuka laana kwa maana msitari wa kwanza wa torati 28 unasema kwamba ''Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;''. Baraka zote ulizoahidiwa zinaweza kukupata kama nguvu ya yakufanikiwa au nguvu yakukurudisha nyuma{laana} kwasababu ya sautu ya MUNGU. Kuna vitu vitatu katika msitari huu ambavyo ni muhimu sana navyo ni:-
  1. Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako,
  2. kwa bidii,
  3. kutunza
  4. kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo,

        Kuna kitu muhim cha kuelewa hapo nacho ni kusikia ssauti ya MUNGU. Hii inaonesha MUNGU anasema nawewe baada na kabla ya kukupa hiyo nguvu. Pili usisikie tu kwa jinsi ya kawaida lakini uwe mtu wakujitaabisha kwaajili ya kusema na MUNGU wako ndio maana kuna neno  bidii hapo. Tatu baada ya kuisikia ni lazima kutunza kwa maana nyingine ROHO ananiambia hapa ni kuchambua ili kuvijua {mtumie ROHO tu hapa ili uwe vizuri zaidi katika kipande hiki}. Baada ya kuvichambua na kuvijua vyote chukua ambayo ni maagizo ndiyo ukayafanye kwama alivyoagiza MUNGU mwenyewe katika kusema kwake. Usitende kwa jinsi ya kibinadam maana itahesabika kama uasi mbele za MUNGU. 
         imeandikwa na MICHAEL BASA 

Jumatano, 15 Machi 2017

MUDA GANI MUNGU ANAFUNDISHA???

kujibu hili swali ni bora kwanza tukawa na uhakika kuwa MUNGU wetu anasema na watu wake aliowaumba kwa mfano wake. Tazama huu msitari .......Akiwapo nabii kati yenu,Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto {hesabu 12:6 }. Hapa kuna kitu cha kujua kuwa BWANA husema kwa njia anayoichagua mwenyewe kwa maana kwa mananbii wa jamii hiyo kachagua njia ya ndoto. Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali{ayubu 33:14}. 
     
 Basi kupitia maandiko hayo tunaamini kwamba MUNGU hunena na watu wake kama yeye vile apendavyo. Naam sasa ni bora tuangalie njia ambazo BWANA anaweza tumia kunena na mtu mmoja mmoja au na kanisa kwa ujumla.anbazo ni:- 
  1. Wazo jipya
  2. Kutumia watu wa kawaida
  3. Kusema naww moja kwa moja
  4. Mafunuo
  5. Ndoto
  6. Manabii
 Hizo ndizo njia ambazo MUNGU amezitumia kwenye biblia kunena na watu wake sana.
     Manabii wametumika kipindi kikubwa cha agano jipya na pia mpaka leo bado wanatumika kwa kutoa mwongozo na wakati mwingine maonyo kwa kanisa na pia kutoa majibu ya maombi yao.  

    Ukisoma ayubu 33:14--16 utajua ni kwanini kwawewe ni lazima uwe unaota ndoto na pia ni lazima uzikumbuke ndoto unazoota na uzijue ndoto zinazojirudia. Maana ndoto ikijirudia inamaana kwamba MUNGU mwenyewe amelidhibitisha kwako neno lake mwanzo 41:32. 

     Pia wazo jipya linaweza kukujia tu kichwani hiyo ppia ni njia ambayo Bwana huitumia kujifunua na kutoa majibu juu ya maombi. 
         Moja ya tatizo kubwa ambalo watu wengi tunakutana nalo ni kuchagua watu wa kusema nao na ppengine hata wa kuwasikiliza. Lakini watu hao hao wanaweza kutumiwa na Bwana kama vyombo vya wewe kusema naye na kuisikia sauti yake kwa upana sana kwa hiyo Bwana anaweza kusema nawewe na wala usijali. 
   Watu ambao wako vizuri kiroho au ambao wamepakwa mafuta hawa huweza kumsikia ROHO akinena wazi wazi kwao mfano wake ni MUSA. MUNGU anaamuaa kunena kwa ishara na watu wengine wote bali kwa MUSA anaamua kusema naye uso kwa uso. kwa hiyo mafuta aliyopakwa musa yalikuwa tofauti na aliyopakwa haruni. Pia mafunuo huja kwa mtu ambayo BWANA hutumia kutoa majibu au kusema na watu wake. 
  
by MICHAEL BASA. 
Inaendeshwa na Blogger.