Jumapili, 29 Mei 2016

KWA KILA DINI

kwa kila dini
 Wote tunajua kua tumbo la mwanamke limeumbwa kiasi kwamba damu ya mama hai-ingiliani na damu ya mtoto aliye tumboni mwake. Hili ni jambo la kisayansi na ndio maana mama mwenye virusi vya ukimwi anaweza kuzaa mtoto asiye na virusi kama hakutatokea mchubuko kwa mtoto wakati wa kujifungua. Na wote tunajua kuwa MUNGU anajua mwanzo na mwisho wa kila kitu. Kwahiyo ni kweli MUNGU alijua kuna siku Adam atafanya uasi na kutenda dhambi.
Na MUNGU siku zote anaziheshimu sheria zake; Na katika uumbaji wake aliweka sheria ya urithi. Yaani kila binadamu anaezaliwa kwa muunganiko wa sperm cell na egg cell lazima arithi sifa za mama na baba (heredity). Kwahiyo kwa njia ya urithi, dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja yaani Adam. Na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwani kwa njia ya urithi, wote wamefanya dhambi hata kama hawakutenda dhambi kama Adam.
Baada ya dhambi kuingia ulimwenguni… Siku ileile MUNGU alikuja na mpango mwingine akasema Mwanzo.3:15 “nitaweka uadui kati yako (shetani) na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino. Na haya maneno ni ya kinabii ambayo Kwa tafsiri ya neno “kichwa”ni utawala na “kugonga kisigino” ni majaribu, mateso au taabu
Ukiangalia vizuri…mwanaume hajahusishwa kwenye huo mpango, bali ni mwanamke peke yake; Kwani MUNGU anasema, “nitaweka uadui kati yako (shetani) na huyo mwanamke”. Kwahiyo ni kwa uzao wa mwanamke tuu bila ya kuhusisha mwanaume. Na kwa njia hii lazima mwanamke awe bikira.
Lakini hata kisayansi yai pekee haliwezi kutunga mimba bila ya Sperm cell. Kwa njia hii pia hata yai halikuhusishwa kutunga mimba. Kwahiyo mwanamke anakuwa incubator tu; kwa ajili ya kukuza mtoto atakae-fanywa kwenye tumbo lake kwa nguvu za MUNGU. Na kwasababu damu ya mama na mtoto hazichangami… mtoto anaezaliwa anakua nje ya dhambi ya asili ya urithi (sinless).
Kwa njia hiyo mtoto anaezaliwa sio mtoto wa mwanadamu, kwani hajahusisha yai wala mbegu ya mwanadamu. Bali kwa uwezo wa Nguvu za MUNGU, mwili unafanyika kwenye tumbo la mwanamke, na mwanamke anakua incubator kwa huyo mtoto. Na kwasababu ni MUNGU ndiye aliefanya hivyo… basi mtoto anaezaliwa anaitwa “Mwana wa MUNGU”. Hata MUNGU alisibitisha akasema “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye” mathayo.3:17’’ na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’’ Mtu kuzaliwa na bikra ndio ishara ambayo hakuna nabii au mtume kutoka dini yoyote aliyeishi hapa duniani alienayo. Nabii Isaya alitabiri; Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana
Sasa kwakuwa dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja (Adam), na mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu kwa njia ya urithi wote wametenda dhambi; Vivyo hivyo kwa kupitia mtu mwingine mmoja, ambaye yupo kama Adam kabla ya dhambi watu wote wanasamehewa dhambi zao na kupata uzima wa milele. (Warumi.8:12-21)
Kama vile dhambi ilivyoingia kwa Mwana wa MUNGU mmoja yaani Adam (Adam hakutokana na muunganiko egg na sperm cell), hatimae watu wote wa egg+sperm cell wakawa na dhambi na mauti… basi tena kwa kupitia mwana mwingine wa MUNGU yaani YESU, dhambi inaondolewa kwa hao watu wote na hivyo uzima wa milele (luka.3:23-38)
INAKUWAJE YESU MWENYE HAKI ASULUBIWE?
Kwamaana imeandikwa “Mtu mwenye haki huokolewa kutoka katika taabu, nayo huja kwa waovu badala yake(Mithali.11:8). Wote tunajua kua Kitendo cha mtu mwenye haki kuamua kupoteza kitu chake cha thamani kwa kupenda, kwa ajili ya kumuokoa yule asie na haki huitwa “sacrifice”.
Sasa sheria hiyo inatimizwa hivi; Huyu mtu mwenye haki (YESU), asiye na dhambi na ambae hawezi kufa kwasababu yuko nje ya dhambi ya Adam… anaitoa haki yake kwa hiari kwenda kwetu, tena alitupatia baraka zake, na kupokea unajisi, na laana zetu zote. Kwani kwenye torati imeandikwa “amelaaniwa yeye aangikwae juu ya mti” Na baada ya kua najisi, Roho wa MUNGU akamuacha hadi yeye akalia “MUNGU wangu MUNGU wangu mbona umeniacha?” kwa mabadilishano hayo… waovu (wengi) wakawa wenye haki, na mmoja mwenye haki akawa mwovu. Kwahiyo Watu (wengi) wenye haki huokolewa kutoka katika taabu (kusulubiwa/mauti), nayo hiyo taabu huja kwa mwovu mmoja (YESU) badala yao.


Mwandishi: IBRAHIM NZUNDA 0754 210 627

Jumapili, 22 Mei 2016

UTATU WA BINADAM( HUMAN DIVINITY)

basaministry
HUMAN DIVINITY
Kutoka kwenye uumbaji kila mtu unayemuona bila kujali ameokoka au hajaokoka amegawanyika sehemu tatu ambazo MUNGU anazihesabu nazo ni 1. roho,  2. mind (soul),  3. Mwili. Kama ilivyoandikwa kwenye  1wathesalonike.5: 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Ili binadamu afanye ya kazi yoyote hapa duniani kwa mafanikio inatakiwa vitatu vyote vifanye kazi kwa pamoja.  Ila kazi ya kiMUNGU inahitaji viwili kati ya hivyo au vyote vitatu; ambapo MUNGU alichagua roho ili iwe sehemu kuu ya kupokea maagizo na kutunza maagizo yake.
Bali shetani hutumia mwili kama mlango wa udhaifu wa mwanadam yeyote ili ayafanye mapenzi ya shetani warumi 7: 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
warumi8: 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
.  Nafsi yenyewe husubiri ni upande upi kati ya roho na mwili unaokuwa na nguvu kwa muda huo. kwahiyo mind (nafsi)  huwa kiunganisho cha mawasiliano kati ya mwili na roho.
Mtu akiokoka anatakiwa roho yake ndiyo iwe na nguvu ya kumiliki na kutawala nafsi (akili) yake, na kwamba mwili uwe unafuata kile roho inataka kifanyike warumi 7: 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
Sasa  mwili, nafsi na roho kwa pamoja huunda utatu wa binadamu.  Utaona kuwa roho inatakiwa ibaki imeungunishwa na muumba wake, na mwili ni kutaka kutenda tamaa za dunia hii  (warumi 8: 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
warum12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu
kwa hiyo kama ilivyoandikwa kwenye  warumi.8:6-7,  mwili nia yake ni kinyume na nia ya roho, hivyo kunakuwa na uadui kati ya mwili na roho. Basi matendo yote ya kidunia ambayo ni ulevi,wizi,uongo, maseng’enyo,uzinzi, uasherati ,kiburi, kutaka sifa,husuda,chuki,uchoyo,kutunza hasira,kushindwa kusamehe na mengine kama hayo yote ni matendo ya mwili na kamwe hayampendezi MUNGU 1petro2:11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Njia pekee ya kuyashinda matendo ya mwili au njia pekee ya kumpendeza MUNGU ni kuiruhusu roho yako kuutawala mwili wako. Na njia pekee ya kuifanya roho yako ipokee maagizo ya muumba wako ni kuruhusu roho yako na ROHO MTAKATIFU kuwa kitu kimoja.
Na jinsi ya kumfanya ROHO MTAKATIFU kuwa kitu kimoja na roho wako ni kumpokea YESU KRISTO aje atawale maisha yako kweli kweli au kwa maana nyingine kumwabudu MUNGU katika roho na kweli (yohana 4:24), kisha baada ya hapo ni UBATIZO WA MAJI MENGI na baada ya hapo ni kumpokea ROHO MTAKATIFU ili aje akufundishe yote yakupasayo (yohana 14:26)


Kila anapokufundisha inatakiwa ukiweke kwenye vitendo hicho alichokufundisha (yakobo1:22). Pia ujitahidi matunda ya ROHO MTAKATIFU yaonekane kwako ambayo ni  upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.(wagalatia 5:22-23)

Mwandishi MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199

Jumapili, 15 Mei 2016

JINSI YA KUDUM KATIKA UWEPO WA BWANA

  1. KUDUMU KWENYE MAOMBI

Kwa watu wengi maombi kwao ni
  •   nikupeleka matatizo yao yanayoitaji ufumbuzi
  • kupeleka shukrani kwa kile alichotenda MUNGU kwenye maisha yao
  • kumsifu MUNGU
ambayo ni moja ya mambo yanayokamilisha ibada lakini maombi yanaenda zaidi ya hapo na kuna mda mwingine MUNGU huongea na watu na kutoa majibu mengi kwa watu wake ambapo huwa ni kuzungumza na mtu na mda pekee kwa wengi ambapo moyo huwa unamwelekea MUNGU  ni kwenye maombi ISAYA 1:18 mungu anataka kuja kusemezana naye bila kujali wewe unadhambi kias gani. Pia MUNGU kwetu ni baba na tunapaswa kwenenda kama watoto wanaopendwa je ni baba gani anayependa watoto wake ambaye hana mda wa kuzungumza naye waefeso 5:1

2 USHIRIKA NA WATU WA KIROHO

Tabia huambukizwa au kurithishwa kutoka mtu mmoja mpaka mwingine na ndio hizo watu husema “nikitaka kukujua wewe ni nani nionyeshe rafiki zako”. Kukaa na watu wa kiroho kwa mda mrefu ile tabia ya kutenda mema huwa unairihi kwasababu zifuatazo:-
  • Kukatazana kutenda maovu
  • Kushauriana kwa neno
  • Kungojea ufalme wa BWANA kwa saburi pamoja
  • Kuombeana pale wanapokuwa na tatizo Zaburi 33:1,

        3.KUSOMA NENO

Biblia iasisistiza sana kwenye kulijua neno maana neno ni kweli kabisaa na kuijua kweli humuweka mtu huru yohana 8:32b  na pia neno linatakiwa kukaa kwa wingi ndani yako wakolosai 3:26 

kwa kujifunza zaidi pitia HAPA
    
         4.KUOMBA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KWENYE MAISHA YAKO

WOKOVU NI SAFARI ambayo inaanzia pindi tu mtu anapookoka na mwisho wake ni kuingia katika ufalme wa mungu ambapo huyo ndio anakuwa ni mrithi aliyekuwa thabiti kutembea chini ya neema ya yesu kristo ambapo kuna watu hukomea njiani na kukata tamaa kwa kuzongwa na shughuli za kidunia na wengine hushindwa kujilinda na tamaa za mwili na kujikuta wametawaliwa na mambo ya uharibifu kama uzinzi nk ambapo hao wote wanahesabiwa kama walioshindwa kuendelea na safari na wala roho wa mungu hayuko kwao 1YOHANA3:9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu..
ROHO WA MUNGU NI
  • MWALIM WA KWELI YA MUNGU

Marko 13:11 Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu   Luka 12:12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.   Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
  •  MLINZI WA ROHO ZETU

2Timotheo 1:14 Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.
  • KIUNGANISHO CHETU NA MUNGU

Matendo 5:32 Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.
2Wakorintho 3:17 Basi Bwana ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
Waefeso 4:30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
  • MWOMBEZI WETU

Warumi 8:27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
2Wakorintho1:21 Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, 22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.
  • KIONGOZI WA WOTE WALIITAO JINA LA BWANA KATIKA HAKI NA KWELI

Wagalatia 5:18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
  •   MFARIJI

Matendo 9:31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
  • MTETEZI WETU KWENYE MATATIZO MBALI MBALI

Luka 12:12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
  •   ALAMA YA WOKOVU

Yohana 16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.


Mwandishi MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199

Jumapili, 8 Mei 2016

IJUE MILANGO YA KUVUKA KABLA HAUJAFA

1)KUIACHA DUNIA
Hii hutokea pindi mtu anapookoka ni kipindi ambacho mtu anatakiwa kuacha starehe za kidunia alizokuwa anafanya pindi ambapo hajamjua MUNGU (non believer) mf uvutaji sigara,ulevi , wizi, uasherati nk
 ufunuo 22: 15
 mathayo 25:17-25
 waolosai 3:5
husumbua sana kwasababu mtu anakuwa katika kipindi cha kugeuka ili kumwelekea MUNGU (translation period) ambayo bado loop yake inakuwa haijavunjika

CHA KUFANYA ILI KUMUOKOA/KUVUKA HUU KWENYE HUU MLANGO
• Kanisa kumuombea yakobo 5:15-16
• Kufanya juhudi katika kuomba wakolosai4:2
• Kusoma biblia kila siku zaburi 1:6
• Kushikamana na watakatifu na kukaa nao karibu

2)KUIKATALIA DUNIA KURUDI MOYONI MWAKO
mtu anakuwa kafanikiwa kuiacha dunia na mambo yake lakini watu awanaomzunguka wanakuwa bado wanamhitaji arudi kuziba pengo na hii huweza hata kusababisha mtu kutengwa na marafiki au hata kutengwa na ndugu
vitu vya kufanya ili kuuvuka huu mlango
• Kujitoa kwa ajili ya MUNGU mathayo16:24,luka9:23,marko 8:34
• Kujitahidi kusahau mabaya yote uliyowahi kutenda na kushikamana na makuu ya MUNGU tu zaburi 60:12, waefeso 2:4
• Kazana kupata zaidi karama za rohoni 1wakorinto 12
• Jaza neno kwa wingi na pia fundisha wengine luka8:39

3) KUITENDA KAZI YA MUNGU
Hili ni moja la eneo ambalo waumini wengi wamefungiwa ambalo uoga wa kutenda kazi ya MUNGU, aibu ya kusimama na kujitangaza kama mlokole pia watu huridhika na kuingia na kutoka makanisani na pia kuzidi kwa kujihesabia haki pasipo kuitenda wala kuitimiza mathayo3:15
Bila kusahau kuwa milango yote unaweza kuivuka lakini huu kuuvuka ni mpaka pale utakapokufa na hakuna kitu Zaidi ya kushikamana na haki ya MUNGU kujitoa kwa kazi ya MUNGU kwa kutangaza injili kwa kipaji ulichopewa na MUNGU marko16:15

JINSI YA KUDUMU NA MUNGU KATIKA HUU MLANGO
• Kudumu na ahadi za MUNGU
• Kufanya jitihada za kuwa na nguvu kwenye ufalme wa mbingu marko12:20 mathayo 11:112
• Kujitahidi kila siku kukuza karama yako 1petro 4:10
• Kujiepusha na makatazo yote pia kujitunza katika ukamilifu wa BWANA warumi 14:16 efeso5:3
• Kujizoeza kupata utauwa(exercising godliness)1timotheo 4:7
• Kushindana na roho za aibu,kukata tamaa,kinyongo,wivu ,majivuno ,na tamaa za aina zote titus 2:7 ufunuo 21:8
• Kuwaombea watakatifu wote walioko duniani wazidi katika Imani na utauwa Waefeso 6:18
• Kutoridhika na hatua uliyofikia wafilipi 3:12
• Kuyafanya maisha yako yawe ya mfano wa ki MUNGU 1petro 1:15 waefeso5:3
Mwandishi MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199

Jumapili, 1 Mei 2016

KANISA KAMA MAKABURI YALIYOPAMBWA KWA NJE NA WAKATI NDANI YAMEJAA MIFUPA NA VITU VILIVYOOZA.

welcome to basaministry
CHRIST’S GOSPEL INTERNATIONAL MINISTRIES..
    Hii si kumwabudu Mungu bali ni kujifariji, kukimbiza upepo, kujidanganya na kudanganyika kupoteza muda bilakujielewa na kutembea katika giza ndani ya nuru. “na hii ndiyo hukumu ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni na watu wakapenda giza kuliko nuru kwa maana matendo yao yalikua maovu” Yoh 3:19.
     Nani kakudanganya kuwa kanisa ni jengo? Hivyo kuingia kwako katika majengo hayo nawe umekua sehemu ya kanisa!!! Kanisa ni mwili wa Kristo yaani wa YESU na hujengwa na watu watakatifu waingiao mahekaluni. Jiulize  je, wewe ni mtakatifu? Je wewe ni sehemu ya mwili wa Kristo? Au unaenda hekaluni kujaza viti na kuuza sura? “Naye ndiye kichwa cha mwili yaani cha kanisa….” Wakolosai 1:18-19.
     Hakuna kitu kibaya kama unafiki,umefika mbali sana maana hata Mungu unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Kumuonyesha mchungaji kuwa muumini wake wakati wewe ni mtenda dhambi haina msaada kwa roho yako. Yesu mwenyewe anawachukia sana wanafiki kama wewe unayejidanganya kuwa mtu wa rohoni wakati wewe ni wa dhambini. “ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa maana mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa nayo kwa nje yanaonekana kuwa ….bali ndani yamejaa mifupa na uchafu wote” Mathayo 23:27-33. Mstari wa 33 “enyi nyoka wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanamu?”
    Acha kuidanganya roho yako ubadilike kuanzia leo maana matendo unayofanya si ya ki MUNGU bali ya kishetani kabisa. Unaenda hekaluni kwa lengo la kujulikana tuu na si kwenda mbinguni, badilika sasa maana Yesu yu karibu kurudi “tubuni kwa kua ufalme wa Mungu umekaribia” Mathayo 3:2.
    Hayo uyafanyayo kwa siri ni matendo ya mwili na watu kama wewe wamewekwa akiba kwa ajili ya ziwa liwakalo moto yaani jehanamu pamoja na baba yao Shetani au Ibilisi. “basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofana na hayo….ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa mungu” Wagalatia 5:19-21. “bali waoga na wasioamini na wachukizao na wauaji na wazinzi na wachawi na hao waabudio sanamu na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti….” Ufunuo 21:8.
    Sikia nikupe maarifa ya kiMungu haya yote unayafanya na unasema umeokoka muongo acha mara moja;
1.       Wewe ni mzinzi mpaka umekua kero kwenye nyumba za majirani zako. (UTAKUFA NA UKIMWI)
2.       Unavaa nguo za wadogo zako au zilizo kuruka hakuna anayependa kukuona ukiwa uchi  (UMEKUWA KAMA MDORI)
3.       Unavaa suruali kata kei(chini ya kiuno chako) kama hauna mgongo…………..Mmh
4.       Lugha yako si Kiswahili wala kiingereza bali ni matusi acha mambo hayo.
5.       Unaishi na wasiwasi kama unakufa kesho, si mpango wa MUNGU ni wa shetani huo.
      Hivyo ni baadhi ya vitu uvifanyavyo na bado unajiita MLOKOLE na unesema utafika mbinguni. Mbinguni si rahisi kuingia kama unavyodhani  badilika dada na kaka yangu.
Yesu anasema hakuja kwa ajili ya wachungaji, wainjilisti, mashemasi bali kwa ajili ya mwenye dhambi kama wewe “Sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi wapate kutubu” Luka 5:32. Nafasi ya kutubu na kusamehewa ipo kwa ajili yako “tazama nasimama mlangoni, nabisha,mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango nitaingia kwake nami nitakula pamoja naye na yeye pamoja nami.
       Kama unashindwa kuacha dhambi na unasumbuliwa na shida yoyote nitafute na YESU atakuweka huru mbali na dhambi kabisa.
TO THE LORD BE THE GLORY.
PRERARED BY FOUNDER  BUNGUBULIHO F.M Phone 0755285414 or 0716453335

WELCOME IN THE FAMILY OF JESUS CHRIST. Forwarded by BASA MINISTRY.
Inaendeshwa na Blogger.