Jumapili, 24 Aprili 2016

KUUSHINDA ULIMWENGU

kuushinda ulimwengu
Yesu kristo aliwahi kusemajuu ya kujipa moyo kwa mtazamo wa kuwa kila kitu cha ulimwengu ni wale wa ufuatao ulimwengu na tamaa zake nao huwapenda na kuwafurahia bali kwa wale wasioupenda au wanaoenda kinyume nao huwachukia na kutamani wasiwepo bali yesu anasema JIPENI MOYO kwamaana nyingine njia uliyoishika haiwezi kuwa katika wepesi wa maisha yako bali kwamaana yeye anayeenda kinyume na ulimwengu huu yeye anakuwa si wa ulimwengu huu yohana 8:23( Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.)kwa hiyo kama wewe si ulimwenguu huu hauwezi kuyatenda mapenzi ya ulimwengu huu ambayo dhahiri ni matendo ya mwili wala si ya ROHO ambayo yapo wagalatia 5:( 19 Basi matendo ya mwilinidhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.)
 Ukiyasoma hayo matendo mengi yanapendwa na watu wa ulimwengu huu lakini ni matendo ambayo kwayo huwezi kuurithi ufalme wa mbinguni . hebu tazamo jinsi tunavyokaa sisi na marafiki zetu jinsi wanavyotushauri je ni mambo ambayo yanatupeleka mbinguni au ni yale ambayo yanatuondolea utakatifu.Na piindi ukiyakataa unaonekana mshamba usiyejua kitu au wa ajabu sana. Namimi nakushauri jipe moyo maana MUNGU aliyetupenda kwaajili yetu akamtoa mwanawe wa pekee ili afe na afanyike ondoleo la dhambi kwwetu yupo karibu zaidi na kwa upendo wake usiokoma. Sisi hatukumpenda yeye bali yeye ndo alitupenda sisi na hakika YESU alipoondoka hakutuacha  tutange tange(kama yatima)bali alituachia ROHO wa MUNGU akae na hao watakaopokea na kuamini INJILI yake yohana 14:( 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.)
yohana 16:(33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.)

Mwandishi MICHAEL BASA(0765 279 697,+255 789 799 199)

Jumapili, 17 Aprili 2016

“TUSI”; A SOUL POLUTER, MENTAL CORRUPTION AND MIND EROSION TOOL

Mtu anaporudia kusikiliza kitu anachokipenda Zaidi ya mara saba, huwa anaanza kikikumbuka hicho kitu zaida ya 92 percent. And it goes directly and become stored to his sub-conscious mind (in the bible we call it heart). Things that are stored in our heart are what controls our actions, our responses, our attitude and our behavior. Hii principle ndio tunayo-itumia wakati tuna-cram vitu vya darasani.
   Sasa because many don’t like cramming, then we used to repeat something several times more than 7 times, so that it could stick in our minds. Hii njia hutumika kwenye matangazo pia. Kwa mfano “airtel yatosha” ni tangazo ambalo lilirudiwa mara nyingi sana kiasi kwamba karibu kila mtu akawa anajua kuwa kuna kitu kinaitwa “airtel yatosha”. Hi njia imetumika kuangusha wengi sana… Samson aliangushwa kwa hii njia kwa kurudia rudia kuulizwa na ampendae.
   Sasa wengi wetu tunapenda sana kusikiliza nyimbo. Na from the above method huwa tunajikuta tunakumbuka hizo nyimbo vizuri sana. We usually repeat to listen the same song several times because we love that song. Now take an example you are listening a song of “Lily Wyne” who his song is full of evil and sinful words. Ndani ya verses anatukana mara kadhaa… na ndani ya Chorus kuna matusi kadhaa. Na hadi nyimbo inaisha, chorus inarudiwa labda mara tatu. Na chukulia labda umeisikiliza na kuirudia mara tatu… kwa maana unaipenda. The results is that his mind becomes highly corrupted and it becomes full of evil words. Then they start controlling that man unconsciously. Now imagine how satan is busy corrupting our minds!.
   Sasa iko hivi, Kitokacho mdomoni mwa mtu ni yeye mwenyewe, akifanyacho mtu ni yeye na aonekanavyo mtu ni yeye. For it is written “as the man thinks in his heart, so is he” and what the man speak is what overflows in his heart. Mtu aongeae huku akiunganisha na matusi ina maana huwaza kwa kutukana pia. Akishanga… hushangaa kwa tusi. Akishtuka hushtuka kwa tusi. Akitaka kuweka mkazo wa jambo Fulani humalizia kwa tusi. Kwa maana hiyo… atafakaripo hutafakari kimatusi matusi. Kimtokacho mtu mdomoni mwake ndicho kilichojaza nafsi yake. Now, ask yourself; can God cooperate with the mind full of evil word and sinful imaginations?
Satan is very weak. Therefore he is busy trying to make God’s people very far from God. He is busy trying to corrupt our mind so that God cannot hear us even if we pray. Hii inafanya mtu ashindwe hata kutumia dakika mbili kuomba. Kwa maana akiomba sana in his heart anajikuta kawaza matusi na sinfull imaginations. Can you imagine how many have been deceived? And in-fact, the life without God also means “busy but not effect-ive”.
As it is concluded by Jesus our Lord that “A good man, out of the good treasure of his heart brings forth good; and an evil man, out of the evil treasure of his heart brings forth evil. For out of the abundance of the heart his mouth speaks. And also it is written “A fool's mouth is his destruction, and his lips are the snare of his soul”.
   Nobody wants to be called a “fool”. Therefore have to guard our mouth and be careful on what we feed our minds. Look at what you like listening… Do they corrupt your mind? kuna watu watajitetea kwa hili… but it is written “There is a way that seems right to a man, But its end is the way of death”. And also it is written that “Death and life are in the power of the tongue”,
    Mwenzako akitoa tusi mdomoni mwake usikasirike…bali muonee huruma. He was not designed that way…Na ikiwezekana muulize hivi “nani anautumia huo mdomo wako? Ni Roho wa Mungu? Ni roho wako? Au ni roho wa shetani?
Written by Ibrahim J. Nzunda.(+255 754 210 627)

Jumanne, 12 Aprili 2016

MFUMO NA UTAMADUNI WA MAISHA YA KILA SIKU YA KIKRISTO (CHRISTIAN CULTURE)



 
1.NENO LA MUNGU
Kwa mteule yeyote anatakiwa kusoma neno la msalaba kila siku na kulitafakari kila mda ili azidi kutenda mema 
WAKOLOSAI 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 
Pia WAEFESO 6:17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

Kuna faida nyingi katika kutunza NENO moyoni mwako nazo ni:-
a. KUJIEPUSHA NA DHAMBI:- ukilitunza neno liitakusaidia kujua kipi kinaruhusiwa kufanya na kipi hakiruhussiwi kufanya ili kumfurahisha muumba wako na pia litakufanya kushindana na shetani na kumshinda kwa maana ukitumia neno point utakayotoa itakuwa na pumzi ya BWANA ZABURI 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

b. KUJUA BARAKA ZAKO ZILIPO:-ukisoma biblia na kuzitafuta ahdi za bwana utagundua vitu vyote ambavyo bwana ameahidi kutupa viko katika neno lake alilotupa na ndiko Baraka zilikofichwa kwa hiyo unapoweka neno lake kwa wingi ndipo unapojua nini cha kuomba kwa mda huo na kwa kazi uliyofanya ZABURI1:1-

c. KUMJUA MUNGU:- MUNGU haonekani wala hakuna mwanadam anayeweza kumuona mungu na akabaki huru lakini kaelezewa katika neno lake takatifu na ppia akatoa roho wake mtakatifu ili kila aaminiye kwa maana nyingine kusikia neno lake na kukubali kupitia neno hili nitashika sharia zako. Na kwakuwa sharia za BWANA zipo katika biblia takatifu kila ashikaye neno ndiye atakayemjua MUNGU kwa kupitia roho wake mtakatifu

d. KUSUKUMIA MAOMBI:- maranyingi tumekiwa tukiomba hasa tunapokuwa na shida huwa tunatumia neno aliloahidi ni vizuri ten asana maana bwana anaposema leteni hoja zenye zenye nguvu inamaana maombi yetu yawe yale ambayo akiyasikia ajue kuwa huyu mtu anahtaji kweli au pale anaposema njooni tusemezane (ISAYA 1:18) 
bila neno lake huwezi kusemezana na mungu kwa sababu anapoongea huwa anatukumbusha kile alichokisema kwa mananbii wake zamani na hayo maneno yapo katika maandiko matakatifu hata ukisoma mafundisho ya yesu alitumia sana neno la manabii na mitume kufundisha
e. KUKUZA HEKIMA YA KIMUNGU NDANI YAKO:-WAEBRANIA 4:12 maana neno la mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

2.MAOMBI.
Ni mawasiliano na mungu wako na hufanywa kwa ajili ya kupeleka shida(tatizo) lako,shukrani au kumsifu. Kuna aina za maombi yafuatayo:-

a. MAOMBI YA KUMSIFU MUNGU:- mungu wetu hushuka katikati ya sifa hili huonyesha  kuwa mungu wetu anapenda kusifiwa kwa ajili hiyo mtu anaweza kufanya maombi ya kumsifu tu mungu 1NYAKATI 29:10-13

b. MAOMBI YA SHUKRANI:-watu wengi huwa tunategemea pindi tukitoa kitu kumpa  mwingine au kutenda kitu kwa ajili ya mwingine huwa tunapenda na tunajisikia vizuri pindi mtu akirudi kushukuru kwa maana ya kiundani zaidi ni kwamba tunafanya akili zetu kujua kuwa bila mimi hilo jambo lingekuwa halijafika na huuwatunajisikia vibaya pindi ambapo mtu anashindwa kukushukuru kwa jambo ambalo nimefanya kwaajili yake ndio maana huwa tunafundishwa kushukuru tokea tukiwa watoto wadogo ili tukue katika njia hiyo. Je MUNGU wetu si zaidi ukimshukuru anajisikia vizuri(be proud of you) na utamfanya atende vizuri zaidi WAFILIPI4:6,WAKOLOSAI 3:15

c. MAOMBI YA KUTUBU:-mtu anapookoka au baada ya kuanguka katika tamaa za dunia hii anapojirudi anatakiwa kutubu makosa yake kwa kinywa chake mwenyewe na wengine pia huwa tunavunja sharia kwa kutojua au kwa kufaham na ROHO anaposhuhudia ndani yetu pamoja na sisi kwamba ni watakatifu au tunahitaji kutubu mfano mwepesi ni mtu aliyeokoka ambaye hata ukimuuliza kama ameokoka anaweza kukataa kwasababu roho inakosa hadhi ya kuwa mlokole ndipo kipindi hiki mtu anapotakiwa kurudi kutengeneza na BWANA MUNGU wake na maombi atakayofanya ni maombi ya kutubu ZABURI 51:1-15 WAKOLOSAI2:18

d. MAOMBI YA UHITAJI:- moja ya sehemu ambayo kanisa huomba kwa bidii ni kwenye mahitaji yao hasa ya kimwili lakini wnasahau kuwa kukua kwa karama na huduma zao ni muhimu zao kwamaana mtakatifu anatakiwa kufanikiwa kama roho yake ifanikiwavyo 2YOHANA1:2 pia hata MITHALI 3:5-8 bado kwenye msitari wa 7&8 kaonyesha uwiano kati ya kumcha BWANA na kufanikiwa kimwili na BWANA MUNGU yupo anasubiri kusikiliza mahitaji yakokupitia maombi ya uhitaji YEREMIA 33:3

e. MAOMBI YA KUWAOMBEA WATU WENGINE:- ni eneo jingine ambalo sehemu a. kubwa limesahauliwa saana hata tukiamua kuomba tunawaombea tu wale wa karibu yetu na siwatakatifu wote WAEFESO 6:18 na jinsi ya kufanya namna hii ya maombi ipo imeelezwa vizuri kwenye kitabu cha 1TIMOTHEO2:1-10

Aina zake:

  • Kwa watu unaowafaham 
  • Kwa watu usiowafaham
Faida za kuwaombea wengine
  • Kubarikiwa
  • Kufanya wengine wasimame
  • Kupata kile ulichoombea kwa mwingine kabla ya yeye
f. MAOMBI YA KUKOMBOA:-haya ni maombi ambayo tunayafanya katika kusaidia watu  wengine kutoka kwenye vifungo vyao vinaweza kuwa vya magonjwa MATHAYO 10:8 au kufunga kwenye maswala ya nchi au kufungua lolote kama vita. magonjwa ya milipuko MATHAYO18:18 kwa maana MUNGU amekupa mamlaka hayo kwa wateule wake yeremia 1:10

3. MAHUSIANO NA WATU WA KARIBU YAKO

a. KUWA MTAKATIFU
b. KUBARIKIWA
c. KUKUZA IMANI


d. KUJADILI NENO 1WAKORINTHO14:26 Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

e. KUONYANA KATIKA NJIA YA BWANA:- Hii inawapasa wote wale walitajao jina la MUNGU mmoja wao akienda kinyume inapaswa kumuonya ili amrudie BWANA sasa kama hamna mahusiano mazuri utamuonyaje?? WAKOLOSAI 1:2

f. KUPIMWA MAWAZO YAKO NA MATENDO YAKO
:-MATHAYO 5:16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

g. KUMTANGAZA MUNGU:- 1PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

h. KUONYESHA UPENDO WA KRISTO KWA WATU WENGINE:
WARUMI 12:9-21
 9 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
 10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
 11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
 12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
 13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
 14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
 15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
 16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
 17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
 18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
 19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
 20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Naam mpenzi msomaji,tumeona kwa sehemu utamaduni halisi na mfumo wa maisha ya kila siku ya mkristo yaani mtu yeyote yule aliyeamua kumpa YESU KRISTO maisha yake na moyo wake na kuamua kuishi kwa kufuata njia zake!
Je,wewe ni mkristo? umempa YESU maisha yako na moyo wako? kama bado fanya hivyo sasa ili uone uzuri wa maisha ya kuishi kuongozwa na yeye na kuenenda kwa kuufuata mfumo wake
ikiwa una swali lolote au maoni usisite kuwasiliana nasi!
MUNGU AKUBARIKI. 

Jumapili, 3 Aprili 2016

MAMBO YA MKE MWEMA KWA MUMEWE

Leo tujifunze namna ya mke mwema anapaswa kuwa kwa mume wake! (kuwa mwanamke wa kiroho,) hii inabeba mambo yafuatayo:

1. kuwa mnyenyekevu ( usimjibu vibaya au kumpandishia sauti mme wako ni

isahara ya kukosa heshima kwa mmeo MITHALI 15:1

2. usitoe siri za ndani za udhaifu wa mme wako kwa watu wengi (marafiki,

family) WAEFESO 5:12

3. kamwe usimfananishe mme wako na wanaume wengine ( mbona mme wa

fulan yuko hivi au anafanya vile )

4. Hata kama huwapendi marafiki wa mme wako usigombane nao acha mme

wako amalizane nao MITHALI 15:13

5. usijisahau majukum yako kwa mme wako hata kama una house girl ( mme

wako amekuoa wewe sio mfanyakazi) MWANZO 2:24

6. kamwe usigawe majukum ya maangalizi ya mme wako kwa MTU yeyote

....mfanya kazi afanye kazi nyingine zote Ila mme wako ni majukum yako

WAEFESO 5:33

7. kamwe usimlaumu mme wako kwann amekuja nyumbani mikono mitupu

mtie moyo kesho atapata TORATI 3:28

8. Jua kutumia pesa vizuri usiwe mharibifu na kutumia pesa ovyo za mme

wako jasho LA mme wako ni LA thamani kupotea hovyo

9. usijifanye unaumwa kwaku mnyima kufanya tendo LA ndoa na mme wako

(mke na ampe mme haki yake....mke hana amri juu ya mwili

wake.....msinyimane) 1korintho 7:3-5

10.Usimjibu vibaya mme wako mbele ya watoto, wageni, au umati wa

watu.....subiri mfike nyumbani mtatue matatizo yenu

11.Hakikisha unaandaa mavazi ya mme wako kila siku....na kabla hajatoka

hakikisha smartness yake kabla hajatoka

12.usiwaache marafiki zako wa kike kua karibu zaid na mme wako usiamin

13.usiharakishe kutoka bafuni wala kwa dressing table hakikisha uko vizuri

siku zote maana huko njee mme wako anakutana na wanawake waliotumia

muda wao bafuni na kwa dressing table ( usijipambe jitunze)

14.Wazazi, marafiki, ndugu, hawana usemi was mwisho kwa ndoa yako

Wamuzi ni wewe na mmeo

15. Usioneshe upendo kwa mme wako kwa wakati akiwa na kitu mheshim na

umtii, kuwa mnyenyekevu na umpende hata kama unamzidi kipato LUKA 21:16

16. Usiwe busy kwa mme wako kumbuka anahitaji umsikilize uwe na mda kwa

jili yake usiwe na ubize anapoongea na wewe acha unachofanya na umjib

usimjib huku unaendelea na mambo mengine

17.Kama umetowa wazo na likaleta mafanikio usijifanye unaakili kumzidi nyie

ni kitu kimoja.

18. Mwanamke mvivu hawezi kujali mme hawezi kujua kama mme wangu

anahitaji kuoga kula n.k

19. Wanaume hawapendi uchafu hata kidogo.....kuwa msafi kuanzia

mwonekano mpaka chumba cha kulala

20.kuwa mbunifu kwa mme wako.......Fanya zaidi vile vitu anapenda

asivyopenda viache Mara moja

21.Usilazimishe mme wako afanye vile unataka hata kama ni

vibaya......usimuombe vitu vya gharama kuzidi uwezo wake....

22.Jua lugha ya kuzungumza na mmeo akiwa anahasira nyamaza au tumia

polite language , ( Tafadhali, naomba, nisamehe, nakupena, Asante)

23.: kuwa mkarimu kwa wageni wote, usibague upande wako!

24.MPE glass ya maji mme wako baada ya kufika nyumbani kama

ukaribisho.....Fanya hivyo hata kwa wageni waingiao na kutoka malongoni

25.Usiwe na marafiki wenye mawazo hasi na mitazamo mibaya na Tania

mbaya zisizo faa kuigwa

26.Ndoa yako ni yathamani kwakadri unavyoithamin, iheshiim na kuilinda

27.Uzao wa tumbo lako ni baraka kutoka kwa Bwana ....wapende watoto wako

na uwafundishe njia iwapasayo MITHALI 22:6

28.Hata kama umri umeenda na mmezeeka usipunguze na usiache majukum

yako kwa mme wako

29.Mwanamke mwenye maombi ni ngao tosha ndani ya nyumba....Omba siku

zote kwajili ya family yako, mme wako na watoto wako....na watu wengine!

Pia angalia kwenye katabu cha mithali 31:10-31. Bwana akubariki

unapoendelea kujifunza. Amina.
pakua pdf hapa

Mwandish; Michael Basa(0765 279 698, +255 789 799 789)
Inaendeshwa na Blogger.