Jumatano, 27 Januari 2016

NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUANGUKA?

kumbuka kwamba BWANA ni mwingi wa hasira na hakuna hata mmoja awezaye kusimama hata sekunde moja kuikabili hasira yake, naye ni mwenye nguvu nyingi na utukufu. Pia ni mwepesi wa kusamehe ndo maana mpaka leo unaona ni kwa neema tu watu tunaishi
ukisoma Yoeli 2:12-13; BWANA wa majeshi anaonesha ni jinsi gani ambavyo anaitunza hasira yake juu yako na anasema umrudie kwa:

1. MOYO WAKO WOTE - MUNGU ni roho, na imetupasa tumwabudu katika roho na kweli (Yohana 4:24). Kwa maana nyingine naweza sema kwamba BWANA wetu anataka mioyo yote mda wote ikae ikimwelekea yeye kwa kumuwaza na neno lake ndo lijaze mioyo yetu (Mithali 4:23)

2. KWA KUFUNGA- Na kwa jinsi hii unaua tamaa za mwili na kuiacha njia mbaya uliyoiendea ili ukadumu katika uwepo wake siku zote. Kambuka hata YESU alifunga siku 40. Tazama pia waninawi ambao walijivika magunia na kufunga ambapo mpaka mifugo haikutoka zizini mpaka pale waliposamehewa

3. KWA KULIA- Juta kwa kile ulichokifanya mpaka kikakutoa mbele ya uso wake ili ukatubu maana hauwezi kutubu kama hujui kosa. BWANA anasema “kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. (ufunuo.2:5)
pili unashauriwa kwenda kicho mbele za BWANA au kwa maana nyingine kwa kujinyenyekeza jiweke mbele yake kwa mda mrefu huku ukiiombolezea nafsi yako kwa kosa ililotenda na MUNGU atakusamehe baada ya kujuta kwa nafsi yako.
ndipo tukutane katika somo jingine la jinsi kudumu katika uwepo wa BWANA maisha yako yote na BWANA akubariki kwa kusoma hiki kipande.
Mwandishi; Michael Basanorare (0765 279 698)

Jumamosi, 23 Januari 2016

NI NYAKATI ZA HATARI SANA!

Shalom:Ingawa watu wengi wanadharau suala hili la kweli; Lakini mjue jambo moja kama ilivyoandikwa “Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”. Tena ingawa hakuna ajuae SIKU wala SAA; lakini tumepewa uwezo wa kutambua majira na nyakati za kuja kwake. Kama Yesu alivyosema, “myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni”. (marko.13:28-29)
Ndugu zangu Dunia inielekea mwishoni maana kila dalili na mambo yaliyoandikwa yanatimia sasa, Niajabu sana kuona kuwa watu wanaendelea kufanya mambo mabaya bila kufahamu kuwa dunia inarudi kipindi cha SODOMA NA GOMOLA INCHI ILE ILIYOCHOMWA MOTO NA KIBERITI (Mwanzo 19:24).
Nimaajabu makubwa kwamba wanyama wote wanatambua majira na nyakati chini ya jua lakini mwanadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu hatambui wala haelewi kinacho-endelea chini ya jua. “Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri” (Isaya 1:3).
Sikia haya yanayofanyika duniani leo na mengine hata wewe huenda unayafanya,, Wasomi watembea nusu utupu na kupigapicha za utupu, Ndoa za jinsia moja zimehalalishwa, wadada kutoa mimba kanakwamba wanatoa taka mwilini, Mauwaji ya kutisha na ugaidi kila kona,dhuruma na ufisadi mkubwa sana, Usaganaji, ushoga na ufilaji mchafu, mziki na ngoma za uchi maeneo mbalimbali. TUSIJIFANYE HATUNA AKILI, HAYA YOTE YAMETAJWA KWENYE BIBLIA NA NDIO DALILI ZENYEWE
ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana imeandikwa “watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake;...” (2Timotheo 3:1).
Jiulize maswali yafuatayo:
 Toka umeanza kufanya UZINZI umepata nini cha kumwonesha YESU atakaporudi?
 Kwa nini huwapendi watu wanaomwabudu Mungu katika roho na kweli! Shituka ndugu
 JE ukifa bila kumwamini Yesu mwenye uzima wa milele, UKAMKUTA HUKO utaweza kuvumilia Moto wa JEHANAMU? GEUKA Mwanadamu
 Pamoja na dini yako umeweza kuacha dhambi na hasa hasa dhambi ya kizazi hiki ya UZINZI na UCHAWI?
 JE unajua kuwa wewe ni mtumwa wa dhambi na hivyo imekupa kibali cha kuwa mtoto wa SHETANI na hivyo ukifa bila kumwamini YESU unakwenda MOTONI?
 JE wewe uliye jificha kwenye nyumba za ibada unazani MUNGU hakuoni!!!!!!!!!!!!!!! YESU amekuona ACHA LEO YESU AKUSAMEHEEEEEEE....
 Je wewe ni shoga mbona unavaa Nguo zilizo legezwaaa? na we MSICHA mbona hizo nguo zimekuluka? acha kuzizaa unajiabisha halafu zinaonesha KUWA UNA MAPEPO YA UZINZI NA UMALAYA.
Ukiyajua haya, niheli uachane na njia yako mbaya ya UZINZI,UMALAYA, ushilikina, matusi NA MENGINE, na kumpokea YESU ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Bwana asema “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa...” tena imeandikwa “ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. (Warumi 9:9-10).
 pakua pdf hapa

PREPARED BY BUNGUBULIHO M. FREDRICK , 0755-285-414

Jumatatu, 11 Januari 2016

ONLY GOD CAN JUDGE ME

pakua pdf hapa
Ukweli ni upi kuhusu hukumu? Je,ni kweli kwamba MUNGU pekee ndiye anayetoa hukumu? Na pia hukumu ni nini?.

Nilipokuwa nasoma biblia nikakutana na mstari unaosema “hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo” (1kor 6:2). Sasa unaweza kujiuliza, je, watakatifu ni miungu? au je watakatifu wapo duniani?.

kama hawapo duniani wako wapi? na kwa muda huu wanafanya nini huko? Imeandikwa “kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu,...” (1kor.1:2). Hapo kuna neno “kwa watakatifu walioko korintho” (ambalo ni jina la hapa duniani), na tena “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao” (zab 16:3). Hapa ndipo unagundua kuwa walioitwa kuwa wana wa MUNGU ndio walio watakatifu na ndio watakaouhukumu ulimwengu. Sasa Je wewe ni mtakatifu ambae unaweka ONLY GOD CAN JUDGE ME?.

Ni kweli imeandikwa “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi” lakini usiishie hapo maana sababu yake imetolewa sehemu nyingine kwa kusema “wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa MAANA WEWE UHUKUMUYE UNAFANYA YALE YALE”. (war 2:1). Kwahiyo kama wewe siyo mtakatifu usihukumu kwani “hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa

Basi amini amini nakuambia, watu wale ambao miili yao ni Hekalu la Roho Mtakatifu ndiyo watakatifu watakaohukumu ulimwengu. Pia hao ndiyo leo kabla hawajatoa hukumu siku ya mwisho ndiyo wanaolitangaza neno la uzima; ili pale watakapokaa kukuhumu uwe unaijua kweli. Na uwe mwenyewe ndiyo umelikataa neno liletalo uzima kwa kufuata matakwa yako mwenyewe. maana imeandikwa “Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?” na tena “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” (warumi 2:27)

Mungu amesema “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”. Basi ndugu yangu nakusihi badilika, ubali hukumu za haki siyo kujivika kiburi cha kwamba MUNGU pekee ndiye anaweza kukuhukumu wakati maaandiko yako wazi juu ya hilo kuwa watakatifu au walioitwa na kutii sheria za MUNGU ndiyo watakatifu watakaohukumu ulimwengu huu.

Ndugu, na wewe pia unaweza kuwa mmoja wa watakatifu ili usihukumiwe kwa hukumu ndogondogo, bali wewe ndiyo uje uwahukumu wale wote wasioamini. Na njia pekee ni kumpokea Yesu Kristo na kukiri kuwa MUNGU alimfufua kutoka katika wafu (war 10:9)
Mwandishi. Michael Basa (0765 279 698 / 0789 799 199)

Ijumaa, 8 Januari 2016

KARIBU KWA SWALI LAKO

kama kuna swali kutoka kwenye maandiko(post) zangu unaweza kuuliza hapa na pia karibu kwa mjadala kadiri MUNGU atakavyonipa neema nitajibu 

Pia unaweza kuchangia kwenye swali lolote liloulizwa na mtu mwingine kwa lengo moja la kukuza injili ya YESU kristo

WIFE & HUSBAND MATERIAL

DOWNLOAD HII PDF

Kuna maarifa ya Ki-Mungu ambayo ukiyakosa yanasababisha ukose au uchelewe kumpata mtu wa kufunga naye ndoa. Mimi mwenyewe nimejionea Mtumishi wa Bwana akitumwa na Mungu kumwambia dada mmoja; Mungu akasema “ulitakiwa kuolewa mwaka huu, lakini kwa kutokujua kwako umekosa watu wawili mpaka sasa” na huyo mtumishi akasema “nakwambia hili ili usije ukakosea tena, kwani Mungu anakuletea mtu mwingine wa tatu sasa”.

Pia yapo mambo yanayomfanya mtu atafutwe au awe anakutana na wale wa hit and run badala ya mtu wa ndoa. Mkaka akiulizwa “unataka uoe mwanamke wa namna gani?, cha kwanza atasema “awe mcha Mungu na mwenye tabia Njema”. Mdada naye atasema “nataka mume mwenye Hofu ya Mungu, anayejua kupenda na mwenye akili za kimaisha”; Hii ni njema, lakini je nawewe uko kama huyo unaemtaka? (Maana Hakika Bwana atakupa wa kufanana naye).

Bwana anasema “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. (gal.6:7-8) .

Kwahiyo kama mwanamke unataka uwe na mwanaume mwenye hofu ya Mungu; Inamaana huyo kijana mwenye hofu ya Mungu lazima atakuwa hataki kutenda dhambi na anaziogopa dhambi, ikiwemo ile dhambi ya kuwaka tamaa. Sasa kama wewe ni dada na unavaa nguo na suruali za kubana, zinawasha tamaa wanaume; utasumbuka sana kumpata mtu mwenye hofu ya Mungu.

Hata kama umeokoka na unanena kwa Lugha; Lakini mavazi yanakugharimu wewe. Kwani kwa kufanya hivyo unawasukumia mbali wenye hofu ya Mungu na kuwavutia wale waharibifu, unawavutia wawaka tamaa, wale watu wa “hit and run”. Usiutumainie mwili kumpata mwenzi wa ndoa, maana Bwana anasema “yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu;” (gal.6:7). Ukitaka kupendwa kwa kuvaa kimitego unaishia kuvuna watu wa “hit and run”

Tambua kwamba; tabia yako, mwenendo na usemi wako ni mbegu kwa wengine na ni matunda kwako. Na kutoka kwenye hayo, anaetaka kuwa nawe anapata picha ya jinsi gani maisha ya ndoa yatakuwa kama ukiwa naye. Bwana anasema “uwe kielelezo…, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi” (1tim.4:12). Maana mtu wa ndoa atakupenda na kutambua kama unafaa kutokana na jinsi unavyo-behave; kwasababu “Mtawatambua kwa matunda yao” (mt.7:16-20)

Kama unataka kumpata mwenzi wa maisha sasa… lazima uwe presentable. Jiandae basi uonekane unastahiri kuolewa au kuoa. Lazima uwe wife au husband material. Ili wale wanaotafuta mke wakikuona moyoni mwao waseme “huyu anaweza kuwa mke” au wadada waseme “huyu anafaa kuwa na mke sasa”. Sio kila wakikuangalia waone bado hujielewi au waone hujiheshimu. Kristo anasema “nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema” (mt:5:16)

Chukulia kama umezaliwa ili uwe mtoaji mali mkubwa kwa ajili ya kanisa la Bwana, alafu ukakataa kuokoka kabla ya kuoa, then ukaoa mwanamke mwenye moyo wa ubahiri; unategemea nini hapo kama ukiokoka baada ya ndoa?. Kwahiyo ni hatari sana kwa kijana kuishi bila wokovu.

Mwanamume imekupasa uwe na Roho Mtakatifu, yaani uwe umezaliwa mara ya pili (born again/kuokoka)(tit.3:3-7). Pili lazima uwe na maono, uijue assignment ambayo ilikuleta duniani. Uzuri wa sura na umbo unayo thamani kwa mwanamke kama anaye Kristo ndani yake, lakini kama Yesu sio Bwana na Mwokozi wake; uzuri wake ni ubatili, tena ni harufu ya uharibifu. Kama ilivyoandikwa “uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa” (mit.31:30)


Mwandishi: Nzunda Ibrahim (0754 210 627)

Alhamisi, 7 Januari 2016

JE, YESU NI MUNGU?

Ndugu Msomaji habari!.

Tunajuwa kuwa MWANGA una asili mbili (dual nature) kwa pamoja ambazo haziingiliani na wala hazitengani. 

"Mwanga ni wave na vilevile ni particle." Na wave ni immaterial lakini particle ni material. 

Na mwanga unazo sifa zote za wave yaani diffraction, refraction, interference n.k. Pia mwanga anazo sifa zote kama particle na tuna-utumia kutengeneza umeme wa Jua (sola power). (kumbuka de Broglie wave-particle duality).

Sasa Yesu amesema kuwa yeye ni MWANGA (LIGHT).
Alikuja duniani katika umbo la binadamu na akawa binadamu kamili (i.e. particle) na sifa zote, wala hakuwa fake, kwani Mungu hatengenezi fake. Ndiyo maana Yesu anasema “hakuna mtu ye yote aliye mwema ila Mungu peke yake” na alilia “Mungu wangu Mungu wangu, mbona umeniacha?” (KUHUSU U-MUNGU NIMEANDIKA AYA ZA CHINI).


Ndio maana imeandikwa “Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama Yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo”(warumi.5:12-19, 1korintho.15:20-22).

LAKINI kwa sababu ana-asili mbili… yote haya hayamfanyi Yesu asiwe Mungu. 

Yesu alipoulizwa “Bwana, tuonyeshe Baba yako yatosha”…Yesu akajibu “Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue?” (yohana.14:9-10). 

Huyu ndiye Yesu ambea pia ni Mungu na aliyesema

“tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.(ufunuo.22:12-13)

Pia imeandikwa
“kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani (Isaya.9:6). 

Na pengine imeandikwa 
“Hapo mwanzo, alikuwako Neno, Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” 
na inamalizia kwa kusema
“Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake. (yohana.1:1-14, 17:4-5, wafilipi.2:6-11). 

Bwana akubariki sana. AMEN

Imeandikwa na IBRAHIM J. NZUNDA (0754 210 627)

 – kupata softcopy Ya Somo Hili Bonyeza Hapa || Kupata SoftCopy Zote Bonyeza Hapa

Jumapili, 3 Januari 2016

DOWNLOAD MAFUNDISHO HAPA!

Ndugu msomaji; sasa unaweza kupakua mafundisho haya yaliyopo kwenye mfumo wa pdf na ukashiriki pamoja na wengine ambao bado hawajapata ujumbe huu na baraka hizi za MUNGU kwa kufuata link hizi hapa chini.

1:SOMO 01: KITOKEACHO MTU AKIZINI

2:SOMO 02: JE YESU NI MUNGU?

3: SOMO 03: KANISA vs DHEHEBU 

4:SOMO 04:  KIPIMO CHA UMASIKINI

5:SOMO 05:  KUOKOKA NI NINI?

6: SOMO 06:  KUOLEWA VS KUOA

7: SOMO 07:  MAMBO YA MKE MWEMA KWA MUMEWE

8: SOMO 08:  WASOMI NA MUNGU

9: SOMO 09:   MTAKATIFU NI NANI?

10: SOMO  10: UTOFAUTI KATI YA MTAKATIFU NA MKAMILIFU

11: SOMO  11: MWONGO NI NANI?

12: SOMO  12:  KUHUSU NDOA 

13: SOMO  13:  NI NYAKATI ZA HATARI SANA

14: SOMO  14:  SAYANSI NA YESU

15: SOMO  15:  THE GOLDEN CHANCE

16: SOMO  16:  UTATU WA MUNGU

17: SOMO  17:  WADADA- KWENDA NA SHETANI 

18: SOMO  18:  WAITING AND DATING by Dr. Myles Munroe

19: SOMO  19:  TUNALINDWA HIVI NA MUNGU

20: SOMO  20:   TUSI- A MIND EROSION TOOL

21: SOMO  21:   UTAJIRI NA KUOKOKA

22: SOMO  22    SADAKA YA UPENDO

23: SOMO  23  ROHO MTAKATIFU


Inaendeshwa na Blogger.